Mbowe hakupaswa kusubiri watu watangaze kugombea uenyekiti bali alitakiwa awe ametang'atabgaza kung'atuka kabla

Mbowe hakupaswa kusubiri watu watangaze kugombea uenyekiti bali alitakiwa awe ametang'atabgaza kung'atuka kabla

Tatizo lake ni mropokaji. Kama kweli ana sifa wenzake si wataona na kukubaliana agombee bila kushambulia Mtu?
Kusema ukweli ndiyo kuropoka na amemshambulia nani katika hotuba yake? Maccm mumerukwa kusikia Lissu anaenda kuwa Mwenyekiti na bado.
 
Kusema ukweli ndiyo kuropoka na amemshambulia nani katika hotuba yake? Maccm mumerukwa kusikia Lissu anaenda kuwa Mwenyekiti na bado.
Mtu mwenye sifa anatangaza nia na kusubiri kampeni. Sasa unatangaza nia na kuisema Chama chenyewe na viongozi wake, sasa hapo unajenga au unabomoa?
 
Lissu anafaa kwa Uongozi lakini si nafasi ya Mwenyekiti. Labda Katibu Mkuu au abaki Makamu MKiti. Kwa msimamo alionao Chama hakitadumu kitafutwa mara moja kwa kukiuka sheria za usajili.
 
Kwa status ya Mbowe anatakiwa kuwa na ajenda ya kustaafu uenyekiti na kualika wengine wagombee bila yeye kuwepo. Na kuwe na tafrija maalum ya kumuaga na kupigia mstari legacy yake kubwa sana katika kuimarisha siasa za upinzani nchini - kwa jasho na damu.

He’s, indeed, a giant of opposition politics in Tanzania during the country’s most turbulent times of multiparty politics.

Kisha waalikwe watia nia wenye sifa wapambanie nafasi hiyo kwa uwazi kabisa. Lisiwe suala la watu wawili au kambi za watu. Tujue kabisa kuwa CHADEMA ni chama cha kidemokrasia cha wananchi (sauti ya wananchi) na sio cha magenge ya kimafia tunayoyaona kwenye chama dola.

Binafsi kabisa ningependa sana kuona watu wenye kaliba (calibre) kama ya John Heche wakigombea. Naamini wako na wengine wengi wanaostahili sana hatuwafahamu tu. Mlango uwekwe wazi. Sio kwa wenye kelele nyingi pekee. It should be a real open process bila mizengwe ya kijinga.
 
Endapo CDM itaangukia ktika mikono isiyo salama, lawama zote zitamwangukia Mh.Mbowe kwani kazi yote aliyoifanya miaka 30 itakuwa sifuri.

Naiona CDM ya Lissu ya siasa za vurugu, siasa za jino kwa jino, siasa za weka chuma weka ugoko. watu watapigwa, vilema wataongezeka na wajane watajaa.

CDM wanatakiwa wawe makini sana, huu ni mtego kwao.
 
Back
Top Bottom