Akiongea na watanzania walioko Marekani, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema suala la mktaba wa Tanzania na DPW ni suala ambalo hata watu wa serikalini hawalipendi.
Akijibu swali la mmoja wa washiriki wa mkutano huo amesema amepata simu kutoka kwa watu wa usalama wa Taifa na serikali wakisema suala la kupaza sauti lifanywe na upinzani kwa kuwa walioko serikalini hawawezi kupaza sauti ambapo itakuwa ni sawa na kupinga maazimio ya serikali.
Mbowe amesema mtu yoyote mwenye akili timamu anajua mkataba wa DPW una tatizo kubwa lakini ukihoji wanaleta propaganda kuwa watu ni wabaguzi aidha kwa mlango wa dini au uzanzibar. Hili suala ni zaidi ya masuala ya dini na utanganyika.
Amesema kwa maslahi ya Taifa wanaoona watu wanapinga wasidhani kuwa wanapinga kwa chuki au wivu.