Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Mimi nilidhani una access ambayo wengine hatuna. Vigogo waandamizi ni binadamu na huwa wanakosea. Ndio maana katika kamati kila upande inapata nafasi ya kuwashawishi waumbe ili wakubali hoja yake. Baada ya hapo mawezi ya waliowengi ndio yanayokuwa ndio msimamo wa Kamati. Nijuavyo mimi katika Kamati kura zote zina uzito bila kujali nafasi ya mpiga kura, ubobezi wake n.k. Ikiwa mawazo ya vigogo waandamizi yanakubaliwa tu hata kama ni minoity basi ina maana kuwa hiyo Kamati imekuwa "animal farm ya George Orwell". Wale wasio vigogo wataona hamna sababu ya kuchangia mawazo yao. Hiyo inakuwa ni cabal. Na Makamu Mwenyekiti inaelekea hulka yake ndio hiyo. Anachotaka yeye ni lazima kiwe ndio msimamo wa wote maana yeye anajua kuliko wengine na tusisahau anatembea na risasi mwilini mwake.Kwa hoja hii mimi si CDM wala sipo hata karibu na ofisi zao. Sijui nini kilijiri lakini nadhani kulikuwa na ku bulldoze waliokataa. Sijui kama kura zilitumika na sijui kama hoja za waliokataa ziliangaliwa kwa ubora. Sijui
Ninachokijua, waliokataa ni vigogo waandamizi ! na hili linaeleza jambo.
Maridhiano ni sawa na upatanisho. Mara nyingi yanafanyika pale pande moja inapoona kuwa mwenye nguvu anamuonea na hamtendei au hakumtendea haki. Kuna mtu atabisha kuwa CDM ilikuwa haitendewi haki? Kuna mtu atabisha kuwa CCM imeshika mpini? Mbowe alikosea nini kutaka upatanisho ambao utawarudisha katika hali ya ushindani na sio uadui?Mazungumzo (dialogue) hutokea kati ya wawili au zaidi katika kubadilishana fikra na mawazo
Maridhiano (reconcilliation) ni upatanishi unaoleta muafaka baada ya pande husika kuhitilafiana
Hili la MARIDHIANO hatukulizua, tumeliazima kutoka kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh FAM
Hili nimelijibu hapo juu. Inawezekana kuwa wakati wa JPM palifanyika majadiliano ambayo walitegemea yatale maridhiano. Nakumbuka Mbowe alienda na viongozi wenzake Mwanza na kumuomba hadharani Rais wa wakati ule wakae pamoja ili kupoza hali iliyokuwepo nchini. Alimuomba kwa sababu alitambua kuwa wao wameshika makali katika suala hilo na mtu pekee mwenye mamlaka ya kupunguza maumivu yao alikuwa Rais. Na hilo lilikuwa linawezekana kwa sababu wakati wa marais waliotangulia waliweza kufanya siasa za upinzani kwa uhuru zaidi.Kwa mujibu wake, kulikuwa na Maridhiano 1, wakati wa JPM ambayo hayakuwa na matunda
Alichokwenda kuongea na Mh Rais ilikuwa kutafuta maridhiano 2 ya kisiasa nchini. Ni kwa mujibu wake
Kwa Maana ya maridhiano hapo juu, tuna maswali; ni pande ngapi zilihitifiana, je zilihitilafiana kwa jambo gani, na wahusika ni akina nani.
Sio consensus. Consensus ( kukubaliana kila kitu) inatafutwa ndani ya chama henye msimamo mmoja na sio baina ya washindani maana pakiwa na consensus hamna ushindani. Lengo la mazungumzo ni kufika mahali ambako mtakubali kutofautiana kwa heshima na amani. Kila mmoja ataheshimu haki ya mwenzake kutofautiana nae. Consensus ingeweza kutafutwa ndani ya chama kwa kujadiliana mpaka wanafikia muafaka unaokublika na kila mmoja wao. Mwalimu alikuwa anasema hivyo ndivyo ilikuwa demokrasia ya kiasili ya kiafrika. Wale wenye mamlaka ya kutoa maamuzi walikaa chini ya mti na kujadiliana mpaka wote wanakubaliana. Ambacho hakusema ni kuwa sehemu kubwa ya jamii ( haswa wanawake) hawakushirikishwa katika majadiliano hayo kwa hiyo ilikuwa demokrasi ya baadhi ya watu.Hapana, lengo la mazungumzo ni kuwa na Muafaka! consensus
Hakukosea. Nimeangalia maana yake na nimetambua hakukosea.Hapa unanioea ! Aliyeleta neno Maridhiano katika kikoa (Domain) ni FAM.
Amelitumia katika kila mkutano. Tafadhali rejelea clip zake
Hapakuwa na consensus kuhusu Katiba Mpya ya Afrika Kusini. Bunge lilipiga kura na walio wengi walikubali kuwa kuna haja ya Katiba Mpya wakati kuna baadhi walikataa wazo hilo kwa sababu waliona hamna haja ya Katiba Mpya wakati wanaweza kuirekebisha iliyokuweko. Hapakuwa na consesus kama unavyodai maana walioikataa waliendelea kuikataa lakini walikuwa wachache kuliko walio ikubali. Kama ilivyokuwa katika Kamati Kuu ya CDM, msimamo wa wengi ndio ukawa msimamo wa Bunge.Of course, baada ya kuwa na Muafaka (concensus) kuhusu South Africa ikiwemo Katiba, iliundwa timu ya Maridhiano(reconciliation) chini ya Askofu D.Tutu (R.I.P) iliyoitwa Truth and reconciliation Commission. Kwa S.Africa Maridhiano yali conclude the process. Kwa FAM alianza na Maridhiano ndio maana tnapata shida ya kumwelewa
Hicho ni kitu cha kawaida. na kwa sababu ya uchache wao hao waandamanaji walishindwa kumzuia asitoke. Walibaki wamebeba wachache tu huku wamebeba mabango yao ambayo alionekana akiyasoma. Huo sio ushindi bali walionyesha insi walivyokuwa inconsequantial.Kuna siku Rais alibadili njia na kutokea uani. Ilikuwa notable . Tu criticise na kutoa credit inapobidi
Kwa nini? Si walikuwa tayari wameruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara? Kwa nini wale waliokuwa hawataki maridhiano wasi elekeze nguvu zao katika kuwahamasisha watu kuandamana? mwenyekiti aliisha onyesha njia. Na watu kama Ntobi na vijana wenzake walikuwa mbele kuwahamasisha vijana wenzao waendelee kudai Katiba Mpya. Na wengi walilipa gharama kubwa kwa msimamo wao? Si unakumbuka yaliyotokea Mbeya? Huyo Mwenyekiti alikimbilia Mbeya aliposikia tu kuna wenzake wameswekwa ndani na wamedhalilishwa! Wakina Ntobi wanajua kuwa siku zote alikuwa nao aliwawezesha kupambana kwa vitendo na sio maneno matupu. Ndio maana wamechukua personal upotoshaji unaofanywa na Lissu pamoja na wafuasi wake. Na wanawajua wote hawa vizuri kuliko sisi na wanajua nani ni genuine na nani mtu wa maneno tu.Haiwezekani kuwa na 'mbadala' wakati Mwenyekiti yupo katika Maridhiano.
Kabla ya kuanza usomaji wa dua katika msiba huo kiongozi wa msiba aliwaasa kuwa katika misiba ya kiislamu hamna kushangilia au kelele za aina yeyote. Watu walipoanza kumzomea Masauni na kumzuia asiseme Mwenyekiti Mbowe aliwaasa wamsikilize kwa heshima ya Marehemu. Ulitaka awahimize waendelee kuzomea ili watakaposhughulikiwa na Tanpol aende kuwapa pole gerezani? Ulikuwa ni uamuzi wa busara maana kwa tension iliyokuwepo waombolezaji wasingeishia kwenye kuzomea tu bali wangeweza hata kujaribu kumdhuru Masauni. Mbowe ni Mwenyekiti sasa kuna dhambi gani kumpa heshima hiyo? Hiyo nayo mnataka kumnyang'anya?Mfano mzuri ni pale Tanga wakati wa Mazishi ya Mzee Kibao (Pumzika kwa amani).
Kuna watu walitaka yule bwana asiongee kabisa! M/Kiti akasimama na kusema '' hapana ataongea'' na yule Bw akasema ''msikilizeni Mwenyekiti wenu, hakusema Msikilizeni FAM''.
Kuchunga ndimi sio kuambiwa wanyamaze? Ni kuwaambia wasitumie lugha ambazo zitaweza kumpa sababu ya aliye upande wa pili kujitoa katika mazungumzo. Au kuwatia ndani hao vijana viongozi na ku frustrate juhudi za chama chake za kufikia kwenye maridhiano.Mafano 2, BAVICHA waliambiwa na M/Kiti wachunge ndimi zao! kwa maana wasije vuruga Maridhiano.
Mhafidhiana maana yake ni mtu "conservative". Hilo sio tusi. Ni mtu ambae si rahisi kubadilika. Sasa kama walikaa pembeni kwa sababu tu wameitwa "conservatives" basi wana matatizo makubwa. Mtu mwenye nia njema angeendelea kujenga hoja yake NDANI ya chama ili Mwenyekiti na wenzake waone wamekosea wapi. Mtu ambae ana amua kusimama nje na kuwabeza waliotofautiana nae ndani ya chama hana nia njema na chama hicho. Mtu Muungwana angejitoa katika nafasi ya uongozi aliyokuwa nao ili asiwe sehemu ya hayo mazungumzo. Mtu mwenye nia njema hafanyi sabotage za wazi wazi.Kutofautiana mitazamo hakufanyi awaye awe Mhafidhina. Neno hilo alilitumia FAM kuwadhalilisha wasiokubaliana naye. Kumbuka ukitaka kumuua Mbwa mpe jina baya kwanzaAngeweza kusema wasioafiki!
Hapo ndipo ukaona wahafidhina wakakaa pembeni jambo unalosema '' waliingia gizani''.
Kwa hiyo amefeli mara mbili tu? Mimi nilidhani mara nyingi kuliko hivyo. Rais wa Zambia aligombea zaidi ya mara tano lakini hakukata tamaa. Mbowe amekifikisha mbali sana chama chake toka alipochaguliwa. Na katika mazingira magumu. na hajakata tamaa. Huo ndio ukomavu. Na tofauti na Lissu najua hata akishindwa atafanya kila itihada kuhakikisha kuwa chama chake hakisambaratiki. Na kikisambaratika atajitahidi kukiunganisha tena. Ndio maana humuoni akitoa maneno ya shombo kwa mwenzake kama wanavyofanya wanaompinga. Na ni wachache sana walio upande wake ndio wamejitokeza kupambana na wapinzani wake kwa hofu hiyo hiyo maana maneno yanaacha donda. Kinachosikitisha ni kuwa Lissu halioni hilo. Anataka ushindi by any means neessary. Huyo ni mtu hatari sana.Wakati wa JPM aliomba maridhiano yakafeli, na sasa ameomba yamefeli.
Huwezi kufeli kila mara ukasema ni ukomavu ukizingatia experience ya miaka 21 kama Mwenyekiti na 33 katika siasa.
Ni lini FAM aliwahi kukabiliwa na sauti nyingi kama sasa! Hii ni rebellion baada ya incessant failures
Ni rebellion baada ya kuona CDM haina msimamo imepoteza uelekeo na inachanganya Wanachama wake
Ni rebellion baada ya kuona same old tricks. Ni rebellion inayotokana na kufanya kile kile kwa def ya insanity
Ukiangalia kwa umakini hizi sauti nyingi zinatoka kwa watu ambao hawana mapenzi na CDM. Zinatoka kwa wale ambao hawakupitia nusu ya machungu aliyopitia Mbowe. Na genius ya CCM ni kumpigia debe Mbowe ili aonekane ni kibaraka wao ili watu wamkimbie kwenda kwa Lissu. Hii ni concerted effort ya wale ambao genuinely wanataka mabadiliko na wale ambao wanataka hayo mabadiliko kwa sababu wanaona Lissu sio tishio. Hii sio grass root rebellion. Ni faux rebellion iliyopikwa kwenye Club House ambako kuna wannabe King makers ambao bado hawajamsamehe Mbowe kwa kuwa"snub".
Tafadhali. You are better than that. Watu ni waoga full stop. Walitoka kwa wingi kwenye maandamano yaliyokuwa na kibali cha serikali. Waliposikia tu kuwa watapigwa kipigo cha mbwa mwizi, wanajeshi watafanya usafi katika eneo la maandamano wakaingia gizani. Ndio maana hiyo confrontational approach haitafanikiwa.Watanzania wengi bado hawataki kupambana na dola. Hivi unadhani pale Magomeni hali ingekuwaje kama angetokeza Lissu na wenzake badala ya kujiweka katika mkao wa kuzuiwa nyumbani. Hiyo ni pamoja na Lema ambae alitakiwa kujua wazi kuwa zitafanyika juhudi kubwa kumzuia kuhudhuria lakinini akapanda ndege siku ya maandamano kwenda kuyahudhuria! Ni farcical kwa kweli.Well, Watu hawakuwa na uhakika kama wakiandamana M/Kiti atakuwepo au ataibukia Ikulu.
Kumbuka kuwa Watu walikuwa Mahakama Kuu wakikabiliana na FFU kabla ya kuona picha za FAM Ikulu.
Kwa hiyo ingekuwa ya mpito tuu. Na baada ya muda huo ingetayarishwa nyingine? Tulichojifunza kwenye Katiba iliyopo ni kuwa kuna umuhimu iwe kamilifu kwa kiasi kikubwa wakati ina pitishwa ili kama kuna ammendments zitakazofanyika ziwe minor.Katiba ingekuwa na miaka 6 tu. Jiulize ya 1977 imefanyiwa amendments ngapi katika average ya miaka.
Ana haki ya kusema hivyo. Hakusema kama msemaji wa serikali. Muda haukuwepo ukiangalia mazingira ya wakati ule. Chama kilitakiwa kiwekeze nguvu katika urekebishaji wa Tume ya Uchaguzi ili uchaguzi unaofuata wawe na mandate ndani ya Bunge. Zitto alikuwa sahihi kwenye hili.FAM kuzungumzia ufinyu wa muda ilikuwa kosa! Yeye hakupaswa kuwa sehemu ya serikali! ni Mpinzani
Muda ulikuwepo lakini Maridhiano yalimtia kibano, akageuka kuwa msemaji wa Kamati ya Maridhiano.
Kwa hiyo hao wanachama watamsusia chama akichaguliwa na Mkutano Mkuu kuwa Mwenyekiti? Aliyeshindwa ataongoza juhudi za kumkataa? Nadhani mna underestimate uwezo wa Mbowe kuwa convince hata wale wanaotofautiana nae sasa hivi kuungana nae kwa ajili ya afya ya chama chao. Lissu akiendelea na fitna fitna itakula kwake. Watu wengi wanakipenda chama chao kuliko mtu yeyote. Tatizo ni kuwa Lissu akishinda ataongoza juhudi za kukibomoa ( pengine bila kukusudia).Nakuhakikishia wakati huu itakuwa tofauti sana. Huko nyuma alikuwa na support ya Bigwigs na Wanachama.
This time hana zaidi ya nusu ya Wanachama. Please kumbuka siongelei wajumbe wa mkutano mkuu.
Yetu macho. FAFO. Walatino na wafanyakazi Marekani wamegundua ukweli huo hata kabla ya Januari 20.
Amandla...
😂 nimeongeza msamiati.
You are welcome.