Sirro hana uwezo wa kumshinda Mungu , ni mtu mdogo sana ambaye siku zake kwenye utumishi wa umma zinahesabika , Mbowe alimshinda Magufuli ndio aje kuwa huyu aliyepewa U IGP na Makonda ?
Na pia hawa watu wanaojipatia fedha kwa madili ndani ya ofisi za umma wanakuaga watu wabaya sana kwa wafanyabiashara halali waliorithi utajiri na Mali za familia na kuziendeleza kwa umakini kama alivyo mbowe ,Manji na Mo.
Hawa watawala na wakuu wa dola wana Mali nyingi ambazo hawana uwezo wa kueleza walivyozipata. Hawa wanaogopa sana katiba mpya wakidhani kuwa inaweza ikatumika kuchunguza Mali zao na uhalali wao.
Wanataka watumie bunduki kurithisha watoto wao madaraka.
Wanawatumia watoto wa maskini kuua maskini wenzao ili kufurahisha utawala wao.
Hata hivyo Chadema imeshindwa kutumia mahakama na sheria zilizopo kufungua kesi nyingi za wazi kwa watu ndani ya dola kuvunja katiba na kanuni za utumishi wao hasa Mwaka 2020 ambapo wengi walichukua formu kuomba ubunge kwa kupitia chama cha mapinduzi. Watu hao bado wapo ndani ya vyombo vya dola na wanajulikana. Kwa nini kesi ya kikatiba isifunguliwe ili mahakama ihalalishe au iharamishe maheshi kujiunga na CCM ili kutumia bunduki zao kukinda vyeo vyao vya juuu na kwa kuilinda CCM?
Jambo lingine ni Kuwa Wapinzani wanaoumia wote watamke siku moja ya kutoa Sadaka kwa kunuia iwe ni kanisani au msikitini au popote kwa Muumba wa wote.
Yaani wamwambie MUNGU wewe uliyeumba vitu vyote ukahukumu kwa haki juu ya watesi wetu wanaotumia madaraka uliyowajalia kuwa nayo . Watoe sadaka na kumlilia dhidi ya waovu waliopewa madaraka na sasa wanatumia nafasi zao kuumiza watu wengine wakati hakuna baya linalofanyika juu yao?
Hivi Samia aliwahi lini kuteswa na Mbowe au hata na siasa za Mbowe tangu kuzaliwa kwake?
Au au Ni nani ndani ya vyombo vya dola aliyewahi kuonewa na Mbowe au kusingiziwa na kufungwa na Mbowe zaidi ya saisa? Kwa nini wamtese MTU ambaye hajawahi kuwadhulumu wao wala familia zao zaidi ya madaraka na siasa za vyama?
Kwa sasa tangu awamu ya sita ianze wanaoiyumbisha nchi ni Watu ndani ya CCM wakishirikiana na Magenge ya wanaojiiata Sukuma Gang iweje Mbowe ndio afungwe wakati wanaomchezea na kuyumbisha mpaka harakati za kupambana na Korona wapo ndani ya CCM ?
Siungi mkono maandamano ya kishabiki ya kupiga makelele ,wala haifai kabisa kufanya fujo .
Kama mtu amechoka starehe za mijini basi aungane na wale wa vijijini tena wale wa zamani mana tumerudishwa nyuma enzi za ukoloni ambapo vijiji palikua na maisha ya kawaida sana yaani mtu anaweza kupanda baiskeli yake au akatembea kwa miguu kwenda ofisini kama ni karibu , asipande bodaboda ,asipande daladala ,asitumie gari binafsi, asivute sigara , afunge kunywa pombe na wanawake mpaka Mbowe atoke,asinunue kwa machinga ambaye anapinga katiba mpya wala duka la anayeshabikia vifo na majeraha ya wanadamu wenzake .
Yaani chinga akimwonyesha mtu bidhaa anapewa ishara ya katiba akionekana anakubali basi auze vinginevyo noo mpaka Mbowe atoke na katiba mpya iruhusiwe kujadiliwa ili wananchi ndio waikatae sio mabilionea akina ndani ya dola wanaowaza kurithisha hii nchi watoto wao ndio maana wanajifanya kuwa wanawapa madaraka vijana. Vijana wao wanapewa ukurugenzi wanalipwa mamiloni lakini wa maskini wanaambiwa wawe na uzoefu wa miaka mitano.
Binadamu aliyeshiba Kumtesa binadamu mwingine kwa sababu tu ya kutaka kusaza na kujimilikisha nchi yote ni jambo baya sana.
Wakubwa wote wameapa kulinda katiba kwa kutenda na kusimamia haki.
Haki ni kwa wote sio kwa wenye madaraka !
Hatutaki kuona Binadamu aliyeumbwa na Mungu anateswa na binadamu mwenzake wakati tumeweka sheria wenyewe ya kuruhusu vyama na upinzani. Katiba Mpya zimejaa kwenye mabohari huko kwenye ofisi za Halmashauri kwa mamilioni ya nakala?
Zimejazwa kwenye mabox bila kusambazwa kwa wananchi . Na zilipelekwa huko na serikali kwa ajili ya kuwapa wananchi wazisome ? Sasa inakuwaje ugaidi kujadili maudhui ya vitabu vilivyochapishwa na serikali?
Kama kujadili Katiba ni ugaidi basi waanze na aliyekua ameruhusu mchakato wa Katiba mpya tena kwa kutumia kodi ya watanzania !!
Kwa nini tusimshukuru Mbowe aliyeamua kupigania mchakato uliotumia mabilioni ya fedha ? Yaani CCM hata makampuni ya umma waliyaua kwa kuweka mbele maslahi ya Chama na makada wao kwa kufilisi Mali za umma badala ya kusimamia uanzishwaji wake na nia yake .
Sent from my TECNO L8 Lite using
JamiiForums mobile app