Mbowe kakodi muziki ,kafunga matenti ,kajaza viti nyumbani ili wanachadema wakamuombe kugombea Tena ! Anafikirisha sana

Si yeye, hao wanaomlazimisha ndio waliofanya maandalizi yote hayo kwa nguvu. Inadaiwa kuwa yeye alijaribu kuwazuia lakini wakamzidi nguvu wakavunja geti wakaingiza hayo ma-tents na viti wakaanda kila kitu bila ridhaa yake
Na Wengine Wakajitolea Kutengeneza Geti Lililovunjwa Ili Mbowe Asisuse Kuchukua Fomu Ya Kugombea Uenyekiti
 
Si yeye, hao wanaomlazimisha ndio waliofanya maandalizi yote hayo kwa nguvu. Inadaiwa kuwa yeye alijaribu kuwazuia lakini wakamzidi nguvu wakavunja geti wakaingiza hayo ma-tents na viti wakaanda kila kitu bila ridhaa yake
Hahahaha du !
 
Sawa. Hao ni watu wanaonufaika na mgongo wake. Hivi unadhani mtu Kama John mrema atataka mbowe aondoke?
 
Mtu anayeenda kulazimishwa anaandaje mazingira ya kwenda kulazimishwa? Anakodisha muziki kabisa na kujaza viti nyumbani kwake ili watu waende kumuomba agombee kweli tumekuwa watoto kiasi hicho ?
Geofrey Mungai anaemsapoti ni bilionia.
Anaweza akatumia pesa kumsaidia mbowe vyovyote.
 
Mtu anayeenda kulazimishwa anaandaje mazingira ya kwenda kulazimishwa? Anakodisha muziki kabisa na kujaza viti nyumbani kwake ili watu waende kumuomba agombee kweli tumekuwa watoto kiasi hicho ?
Nani alikuambia lisu hakujaza ukumbi mlimani city bila kutumia pesa kuwahonga
 
Na yule aliYealika watu akawalipia nauli kutoka huko Bara halafu akakodi na ukumbi wa Mlimani city kutanga nia akisema anaungwa mkono na watu wengi mbona hamsemi ?? Wale watu waliota kuwa jamaa atatangaza nia yake pale mlimani city mpaka wakafunga safari kuja ??? acheni hizooo !
 
Siasa za ujanja ujanja hizi, ndio marais wengine wapo madarakani miaka 20 sasa kwa kujidai wanaombwa wasiondoke.
 
Mtu anayeenda kulazimishwa anaandaje mazingira ya kwenda kulazimishwa? Anakodisha muziki kabisa na kujaza viti nyumbani kwake ili watu waende kumuomba agombee kweli tumekuwa watoto kiasi hicho ?
Huu ujinga alikuwa anafanya Lowassa pia, kumbe Mbowe naye akili zile zile! Mbowe atambue ikifika wakati wa mabadiliko ni wa mabadiliko tu. Inabidi ujiulize ilikuwaje apange viti nyumbani kwakwe wakati hajui idadi ya wahudhiriaji?
 
Si bora Mbowe aliekodi mziki nyumbani kwake ! Je yule aliekodi ukumbi Mlimani city ! Nani katumia pesa zaidi ?? Na wale wapambe waliotoka mikoani nani aliwalipia nauli mpaka hapa Daslaam ? Pesa za malazi na chakula hakuwapa Lissu ?? Je Lissu alitumia gharama kiasi gani ?? Kwa nini anatafuta uongozi namna hiyo ?? sio tamaa ??
 
Mtu anayeenda kulazimishwa anaandaje mazingira ya kwenda kulazimishwa? Anakodisha muziki kabisa na kujaza viti nyumbani kwake ili watu waende kumuomba agombee kweli tumekuwa watoto kiasi hicho ?
Nyie CCM kwanini mnaingilia siasa za vyama vingine wakati ccm hali inazidi kuwa mbaya.
 
Si yeye, hao wanaomlazimisha ndio waliofanya maandalizi yote hayo kwa nguvu. Inadaiwa kuwa yeye alijaribu kuwazuia lakini wakamzidi nguvu wakavunja geti wakaingiza hayo ma-tents na viti wakaanda kila kitu bila ridhaa yake
Mwamba Mbowe ajichunge na Machawa.
 
Ha ha ha siasa bana,namshauri Mhe Mbowe hasigombee amefanya makubwa sana kwani ataheshimika sana sana.ahachane na wapambe wanakula kwa mgongo wake
 
Back
Top Bottom