Haya mambo wakati mwingine nikiangalia chanzo chake ni propaganda nyepesi za lumumba tu zinawayumbisha wasiojiamini.
Maneno kama Mbowe amesalimu amri, amenunuliwa, ni afisa wa TISS, na mengine ni vitu vya kuchekesha sana.
Kila mtu anafahamu msimamo wa Mbowe akiwa gerezani mpaka alipotoka, nani waliomtoa na walimtoa akiwa na msimamo upi, sasa pressure ya kuogopa mazungumzo inatoka wapi?
Oooh Mbowe ni TISS, sasa kama angekuwa mwenzao wangehangaika kumfunga kila wakati si wangempa maelezo tu afanye nini? na kwa kizazi hiki sio rahisi kuwadanganya wengi kwa wakati mmoja, atashtukiwa tu.
Mazungumzo muhimu yawepo, kuanzia hapo ndio ramani nyingine ianze kuchorwa, hapo ndipo mwanasiasa atakuwa na "guts" za kwenda kwa wananchi awaambie kwa upande wangu nilifanya moja, mbili, tatu, hawakujibu; sio kususa, unasusa halafu wananchi wakikuuliza ulifanya nini utawajibu kitu gani?
Kususa ni siasa za kioga, za wasiojiamini na waviziaji, wanaotaka kutumia kila jambo kwa manufaa yao binafsi badala ya manufaa ya watanzania kwa ujumla wao.