Nchi zote duniani huhitaji chama imara cha upinzani kinachoweza saidia serikali iliyopo madarakani kutawala vizuri.Vyama vya upinzani imara huwa ni jicho la pili la serikali kuishitua endapo kuna madudu ndani ya serikali ambayo Raisi au serikali yaweza kuwa hayana taarifa nayo.Pia wafadhili wan je hupenda kuwepo chama pinzani imara kinachoaminika katika nchi ili kuwa jicho lao (WATCH DOG) ya kuangalia kama misaada yao inatumika ipasavyo.
Madudu hayo yaweza kuwa kashfa mbali mbali za ufisadi nk.Chama pinzani chaweza yafichua kupitia wabunge wake kulipuka bungeni n.k
CHADEMA kwa miaka Zaidi ya 20 kilijipambanua kama chama pinzani imara chenye dhamira ya dhati ya kupambana na ufisadi.Kiasi kuwa kikaaminiwa na wananchi wakawa wako tayari hata kukipelekea hati za siri za watu kama Lowasa na wengineo ili wazifanyie kazi.Na wao wakawa waaminifu wakawa wakilipuka bungeni na mikutano ya hadhara hadi baraza la mawaziri likavunjwa mara kibao kwa sababu ya hoja za ufisadi za CHADEMA bungeni.
Wafadhili nao wakatokeaa kuwaamini sana tena sana CHADEMA wakijua kuwa ni chama hodari na kilichodhamiria kupambana na ufisadi kiasi kuwa ripoti za CHADEMA za ufisadi zilipowafikia wafadhili zikiwa na majina ya akina Lowassa nk, wafadhili waliwasikiliza wakazuia misaada ya mabilioni ya pesa zikiwemo za madawa mahospitalini na za kuboresha sekta ya afya na elimu wakitaka suala la ufisadi wa watu kama Lowasa limalizike kwanza ndipo pesa zitoke
Baada ya Tanzania kunyimwa pesa za wafadhili zikiwemo za sekta ya afya na elimu wagonjwa wengi wakaanza kuwa wanalala chini na dawa zikaanza kuwa hazipo mahospitalini,watoto wakawa wanasoma wamekaa chini na serikali kushindwa kuongeza ubora wa elimu sababu ya uwezo mdogo wa serikali.
Tatizo la huduma za afya na elimu zilipoanza kudorora CHADEMA wakaanza kampeni kusema serikali ndio inayosababisha yote hayo wakati ukweli ni CHADEMA ndiyo iliyosababisha wafadhili wasimamishe misaada kwa tuhuma za kusema akina Lowasa mafisadi wakubwa wanazibomoa pesa zao.
Kama kuna chama kilichowasaliti na kuwaumiza watanzania ni CHADEMA.Watu wameumia sana kwa huduma mbovu sekta ya afya na elimu kwa sababu ya CHADEMA .CHADEMA kinatakiwa kiwaombe radhi watanzania walioumia kwa huduma mbovu za afya na elimu zilizosabisha hadi vifo kwa wengine baada ya wafadhili kusimamisha misaada kwa umbeya uliopelekwa na CHADEMA kwa wafadhili uliopelekea misaada ya kibajeti kusimamishwa.Wasizunguke tu na Lowasa wawaombe radhi watanzania kwa hasara waliyowatia kimaendeleo ya afya na Elimu.
Ndio maana nahitimisha kwa kusema mgombea Lowasa wa Chadema ALISHINDWA KUPITA KWA Kuwa CHADEMA kimelaaniwa na wale walioathirika na huduma duni za elimu na afya zilizosababishwa na kukosa hela za wafadhili.Laana ya wagonjwa walalo chini,na wakosa dawa na wale watoto wakaao chini bila madawati na kusoma kwenye nyumba za nyasi,Na walimu wafanyao kazi mazingira magumu ziliwafanya CHADEMA washindwe sana safari hii kuanzia ubunge,udiwani hadi uraisi.
Hili la MCC CHADEMA wamechangia sana kuhujumu ili pesa za wafadhili zikosekane na huduma zishindwe kufanyika halafu wao ndio utakuta baadae wanapita kubwata ona Umeme hamna ni CCM hao!! Wakati wao wamehusika kuchonga MCC.
Hebu fikiria MCC inaweza shupalia kuwa haitioi hela sababu za wale vijana wa CHADEMA na Kituo cha haki za binadamu waliodakwa na kufunguliwa mashtaka.Kesi iko mahakamani hivi MCC hawajui utawala wa sheria hadi waamue tu wenyewe kutoa hukumu kuwa serikali imekosea? Si wangesubiri maamuzi ya mahakama.Hapa wazi kunaonyesha kuna mkono wa CHADEMA.Hivi au inawezekana hiyo software ya kuingilia Uchaguzi ya hao waliokamatwa ilinunuliwa na kufadhiliwa na MCC? Kwa nini MCC wasisubiri maamuzi ya mahakama?
Zanzibar pia kuna malalamiko kuwa kuna vituo vinaonyesha wapiga kura walikuwa wengi kuliko waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.Inaonyesha wazi kuwa kule pia vijana wa IT walichezea mtandao wa ZEC kwa kuungilia.MCC kuna kitu wanaficha lakini yawezekana mtandao ule wa kuingilia matokeo ulikuwa wao.Hatua wanazochukua unaziona kabisa ni za PRO-UKAWA na zinalenga kwenye IT zaidi.MCC nao wawe wakweli.Kuna kitu hawako wazi mahali.