Mbowe: Kukosa pesa za MCC Inachafua jina la nchi ktk medani za kimataifa

Ungejiuliza kwanza bajeti ya nchi yako iliyopitishwa na wabunge wako wa CCM ambao walikuwa zaidi ya 80% bunge LA bajeti, bajeti hiyo inaonyesha utegemezi in % ngapi halafu utafakari watumwa wa akili ni akina nani.

Napata tabu kukuelekeza katika hili ,kifupi hakuna nchi isiyojiendesha kwa misaada au madeni- ni tafsiri ya hiyo 'misaada' ndio inayotufanya nchi za kiafrika zionekane kama ombaomba wa misaada. Nchi yoyote ikiingia vitani au kupata msukosuko wa kiuchumi huomba isaidiwe.
Hapa kuna maelezo yanayoweza kukupa upeo wa maswala ya misaada na madeni. Deni lililotokana na msaada wa kivita lilochukua miaka 100 kulipwa... kati ya marekani na uwingereza. deni limemalizwa mwaka huu 2015.
First World War debt paid off | UK | News | Daily Express
 
Ukiona unaamini kuwa huwezi kujikwamua kwenye matatizo yako mwenyewe kama umasikini wetu bila MCC anza kijihurumia. Ni lini msaada umewahi kumaliza shida za watu.
Jifunze kufikiri vizuri.
 

Una akili za kutosha ndugu yangu Ila hawa malofa na manyumbu hayawezi kukuelewa kama alivyo mwenyekiti wao tapeli aliyehamishia hela ughaibuni akisubiri uchaguzi wa damu halafu yeye na familia wasepe. MCC kwendeni zenu na hela zenu za Freemason. Mungu ametupa Mali za kila aina tutazitumia hatuhitaji misaada ya kafara za damu kwa ajili ya kuwafurahisha wakina Mbowe
 

achana nao mkuu....hata hizo hela zao hatuzihitaji.......yan kwao rais ilikuwa awe lowassa na ndiyo maaana walijazana hapa tz kiba eti kushuhudia uchaguzi.......wakaondoka mmoja mmoja bila kuaga.......shame on them!!
 
Ukiona mtu anashabikia wazungu muogope kama ukoma. Misaada unaiua uchumi.
Sio kweli kwamba misaada inaua uchumi. Usijifariji kabisa dada nchi yetu bado ni masikini na inahitaji misaada ili kufanikisha baadhi ya mambo. Au unapinga kwa sababu ni mbowe ndo kasema?
 
Jana ilikuwa rushwa/ufisadi, leo Zanzibar na sheria ya mtandao, kesho utawala bora na keshokutwa haki za binadamu na ushoga.
Wawe sawa au wakosee bado sisi ni nchi huru tunatakiwa tutatue matatizo yetu wenyewe.
 
Ukiona mtu anashabikia wazungu muogope kama ukoma. Misaada unaiua uchumi.
Sio kweli, hata hao wazungu wanakopa saan tu. What important is proper allocation and redistribution.
 
Tanzania sasa haihitaji pesa ya aina ya hizi za MMC.

Serikali ya JPM izungumze na wachina na ikope pesa hizo kugharamia miradi yake huku ikilipa deni hilo kwa riba yenye nafuu kuwa kabisa hata kwa miaka 15 au 20 sio mbaya.

Zimbabwe na Afrika Kusini wanafanya hivyo na wanaendesha nchi zao bila shida kubwa.

Wachina hawana minyororo kwenye pesa zao ni makubaliano tu na kazi inaanza.

Hizi pesa za kuja na masharti hazina tija sana.
 
Tatizo magufuli sio mwanadiplomasia, hajui afanye nini zanzibar, kakaliwa kooni

Walishajipanga kugawa raslimali zetu sasa imekula Kwao mafisadi nguli wanaotumia siasa na unyonge wetu kujitajirisha. Huyo mbowe haoni aibu hata aibu kuja mbele ya hakiki.kutendo chao cha kumkaribisha majizi yatawachizisha tu .
 
Ukawa hamna uzalendo kabisa yani mnazuia misaada subiri uchaguzi tuwakomeshe
 
Mbowe sisitiza kulipa kodi na kukusanya kodi. Mambo ya kutegemea ufadhiri yamepitwa na wakati. Upinzani mje na ajenda zenye tija kwa taifa. Siyo kuhamasisha uombaomba.
 
Nilijua tu maadam Dr Slaa hayupo CHADEMA kitakosa hoja za kueleweka za kuongea,Dr Slaa angekuwepo angemtia moyo Dr Magufuli kutoogopa kukosa fedha za MCC kwasababu nchi yenyewe ina fedha za kutosha za kujiendesha.Dr Slaa alikuwa anapinga misaada kwakuwa ilikuwa inatengeneza mental slavery na entitlement yaani kuhisi kama mna wajibu wa kufanya chochote mtakachoambiwa na wafadhali wenu kama vile kukubali ndoa za jinsia moja au kusaini mikataba mibovu yenye kuliingizia taifa hasara;pamoja na kujiona mna haki ya kuendelea kuomba misaada (entitlement). Mbowe anapaswa kufahamu kwamba kumtaka rais aendelee kukumbatia misaada ni sawa na kumshauri rais aendelee kuuweka uhuru wa nchi wa kujiamulia mambo yake yenyewe rehani.Yeye kama kiongozi wa upinzani alipaswa kumwonyesha rais alternative ya kujipatia pesa za kuiendesha bila kutegemea misaada,misaada ina gharama zake.
 
Mbowe ni bepari, kibaraka anayeunga mkono utegemezi...
CCM inaamini katika Ujamaa na Kujitegemea, umaskini jeuri...
Anachanganya mambo ya MCC na maslahi yao ya chama... Sioni hoja!
 
Watu wa aina ya Mbowe ndo hugawa nchi zao kwa wakoloni...

Uko sawa, Wachaga waumini wa Sera ya majimbo waliukubali ukoloni wakati wenzao wakipambana nao kwa hasira. Ni jambo la asili..
 

Nafikiri kuna kipengele naweza kutumia na kukushitaki kituoni kwa kunidhalalisha mtandaoni kama mtu mweusi.

Naogopa hata kutumia vi emoj kusema jinsi ulivyonikuna.Kwangu hilo ni tusi, kama mtu mweusi.

Anyways, "white man can't jump"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…