Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwa kwenye mahojiano na BBC amesema;
"Leo Mbowe wa 2025 nina uwezo mkubwa wa kiakili, uzoefu wa kunitosha, nguvu, lakini zaidi nina adhma, dhamira, nina ndoto, nina ndoto ninayotaka kuifikia, kuna kitu nataka nikisukume. Utafika tu wakati ambako (nitapumzika). Hata mimi nimeshatangaza, sidhani kama baada ya kipindi hiki nitakwenda tena kwenye kipindi kingine. Kwamba mimi nimefanya mambo makubwa na wangetamani nipumzika, hiyo huruma inatoka wapi?
"Lakini, siyo kweli kwamba kila damu changa ina uwezo bora kuliko damu ya zamani, hiyo nayo ni dhana potofu, kwasababu ni udhalilishaji vilevile. Katika maisha haya hakuna kitu muhimu kama uzoefu. Siwezi kukimbia kuondoka wakati hatujakamilisha ndoto yetu, tuna ndoto. Binadamu tunafanya kazi kwa maelngo na malengo ni ndoto.
Baada ya kuambiwa ndoto hiyo anaweza kutimizwa na wengine kwenye chama, Mbowe akasema;
"Sahihi, lakini kiongozi mwanandamizi anayeongoza kuitafuta ndoto huwezi kukimbia katikati ya vita, hii ni sawa sawa na vita. Tuko porini tunapigana vita tunautaka uhuru wa nchi yetu. Siwezi nikawaacha wenzangu kwenye mapambano nikakimbia kwasababu nimekaa miaka 20"
Ndoto ipi mbona hasemi anachopanga kufanya hii miaka 5? Cha ajabu anasema "sidhani" kama nitaendelea tena baada ya awamu hii? Kumbe sio kuwa atakang'atuka!! bali hadhani kuendelea?
Huyu ulevi wa madaraka umemzidi, yaani anataka kubaki chairman hata bila sababu za kiutendaji ila title tu.