Pre GE2025 Mbowe: Kuna Watu wanasema Nina mgogoro na Tundu Lissu nawaambia Watasubiri sana, Chopa inaanza operation Karatu na Nitakuwa na Tundu Lissu!

Pre GE2025 Mbowe: Kuna Watu wanasema Nina mgogoro na Tundu Lissu nawaambia Watasubiri sana, Chopa inaanza operation Karatu na Nitakuwa na Tundu Lissu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe amesema wale wanaodhani ana mgogoro na Tundu Antipas Lissu na wanasema CHADEMA imepasuka Watasubiri sana.

Mbowe amesema Chopa inaanza operation Jimbo la Karatu na ndani ya Chopa atakuwemo yeye Mbowe na Tundu Lissu.

Mlale Unono 😃😃🔥

View attachment 3018963

Credit: Vitus Nkuna Ukurasani X

Pia soma: Kuelekea 2025 - Ni kweli Mbowe hawataki Lissu, Heche, Lema, Msigwa na Wenje ndani ya CHADEMA?
Mr Mbowe na chadema kama chama , ccm mpaka sasa imetapatapa , nafikili sio vyema mwenyekiti. M/ mwenyekiti wote kua kwenye chopa moja mnaweza peana zam au achana nayo pia mkapiga ardhi kwa ardhi
 
Ndiyo lakini ni Soviet era aircraft - extremely old and probably with obsolete technology and not airworthy. Waangalie chopa wanazotumia zisiwe zimechakaa kama hayo mabati yaliyoliwa na kutu katika hiyo picha...
Hiyo ndege ilitengenezwa na kampuni ya Dornier ya Ujerumani siyo usoviet ingawa upo sawa ilitengenezwa wakati wa Soviet error 1989
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe amesema wale wanaodhani ana mgogoro na Tundu Antipas Lissu na wanasema CHADEMA imepasuka Watasubiri sana.

Mbowe amesema Chopa inaanza operation Jimbo la Karatu na ndani ya Chopa atakuwemo yeye Mbowe na Tundu Lissu.

Mlale Unono 😃😃🔥

View attachment 3018963

Credit: Vitus Nkuna Ukurasani X

Pia soma: Kuelekea 2025 - Ni kweli Mbowe hawataki Lissu, Heche, Lema, Msigwa na Wenje ndani ya CHADEMA?
---HAKIKA MBOWE ANA HEKIMA SANA, AMETUMIA BUSARA KUUFICHA MPASUKO ULIOPO, HONGERA MWENYEKITI.---
---Hekima na janja nyingine ya mbowe, anafahamu "akitua na helicopter, ni lazima wanavijiji watajitokeza kushangaa helicopter, ndipo hapo hapo huwajaza ujinga"""
 
baada ya mivumo, minong'ono, kauli na hofu ya mgawanyiko na mpasuko ndani ya chama kutanda katika kipindi cha hivi karibuni...

Baraza la wazee chadema (bazecha) limeshindwa kuvumilia hali hiyo na kuamua kujitosa na kuingilia kati hofu, taharuki na sintofahamu iliyotanda ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema, ili kujua na kubainisha mbivu na mbichi baina ya mafahali hawa wawili waandamizi ndani ya Chadema, dhidi ya yanayosemwa mitandani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kutokuelewana kwao, kunakochochea mgawanyiko na kuibua makundi ndani ya chama...

huu ndio umuhimu na maana ya kua na wazee wa chama kwenye taasisi kama hizi, kutuliza hali ya hewa, mnyetishaji alidokeza na kuendelea kusema,

wazee hao wa chama, wameahidi kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari na kueleza ukweli watakao baini baada ya kukutana na viongozi hao, na kukirejesha chama kwenye reli...
alihitimisha hivyo mnyetishaji....

Je,
jitihada hizi za wazee na baadhi ya viongozi wa dini wanaoiunga mkono chadema, zitazaa matunda na kurejesha matumaini kwa waliokata tamaa ndani ya Chadema?

ni suala la muda tu...,
ni vizuri kua wastahimilivu na wenye subra wakati mageuzi katika siasa za vyama Tanzania, yakishika kasi na kuchukua mkondo wake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu 2024, na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2025....

tutaona mengi, tutajifunza mengi, tutajua, tutaelewa na kufahamu mambo mengi mno kisiasa mpaka kufikia uchaguzi mkuu 2025.

na hii ndio afya, uhuru na uhai wa demokrasia ya vyama vingi kwenye ulimwengu wa sayansi na Technologia ..

usiondoke kwenye ukurasa huu muhimu sana na jukwaa hili makini sana la siasa🐒
 
Mbowe anakwepesha kwa hekima zake lakini fukuto ni kubwa kweli, hongera mbowe, kwa hekima zako, si kila jambo ni la kuanika katika hadhara, japo lissu haendi na miiko na maadili ya chama lakini umekuwa ukitumia hekima.
 
Lissu asikubalii, safarii atapatwa na wa chamani kwake, mwaka ule risasi zilishindwa, safarii hii chopa itamuondoa.

Lissu awe makini, asituke mapemaa, huu ni mtego. Aaaah
Bora,mimi nimetahadharisha,CHADEMA wamenitukana mnoo yani kwenye pm yangu.nimewaacha tu,yawezekana hawana hela ya kuchinja mbuzi leo.
 
WAKIPANDA HELICOPTER WAPANDE WOTE, WAKISHIUKA WASHUKE WOTE, ASIAMBIWE MMOJA ATANGULIE KULE.... HALAFU MIMI ITANIFUATA 😁😁😁 (Tom-mbowe & Jerry-Lissu)
 
Back
Top Bottom