baada ya mivumo, minong'ono, kauli na hofu ya mgawanyiko na mpasuko ndani ya chama kutanda katika kipindi cha hivi karibuni...
Baraza la wazee chadema (bazecha) limeshindwa kuvumilia hali hiyo na kuamua kujitosa na kuingilia kati hofu, taharuki na sintofahamu iliyotanda ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo chadema, ili kujua na kubainisha mbivu na mbichi baina ya mafahali hawa wawili waandamizi ndani ya Chadema, dhidi ya yanayosemwa mitandani na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu kutokuelewana kwao, kunakochochea mgawanyiko na kuibua makundi ndani ya chama...
huu ndio umuhimu na maana ya kua na wazee wa chama kwenye taasisi kama hizi, kutuliza hali ya hewa, mnyetishaji alidokeza na kuendelea kusema,
wazee hao wa chama, wameahidi kuzungumza na umma kupitia vyombo vya habari na kueleza ukweli watakao baini baada ya kukutana na viongozi hao, na kukirejesha chama kwenye reli...
alihitimisha hivyo mnyetishaji....
Je,
jitihada hizi za wazee na baadhi ya viongozi wa dini wanaoiunga mkono chadema, zitazaa matunda na kurejesha matumaini kwa waliokata tamaa ndani ya Chadema?
ni suala la muda tu...,
ni vizuri kua wastahimilivu na wenye subra wakati mageuzi katika siasa za vyama Tanzania, yakishika kasi na kuchukua mkondo wake kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa baadae mwaka huu 2024, na uchaguzi mkuu mwaka ujao 2025....
tutaona mengi, tutajifunza mengi, tutajua, tutaelewa na kufahamu mambo mengi mno kisiasa mpaka kufikia uchaguzi mkuu 2025.
na hii ndio afya, uhuru na uhai wa demokrasia ya vyama vingi kwenye ulimwengu wa sayansi na Technologia ..
usiondoke kwenye ukurasa huu muhimu sana na jukwaa hili makini sana la siasa🐒