Pre GE2025 Mbowe: Lissu kuhutubia Taifa ni kukosa nidhamu na kufanya kazi isiyo yake

Pre GE2025 Mbowe: Lissu kuhutubia Taifa ni kukosa nidhamu na kufanya kazi isiyo yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Freeman akihojiwa na Crown FM leo Januari 06, 2025 amesema...

“Unaweza ukanitukana tusi lolote halitanitoa katika focus ninachosema sio kwamba nina uhakika wa ushindi kwa sababu ninakubalika na watu..nani asiyekubalika?”

"Kwa mfano nikupe mfano rahisi nimemsikia majuzi ndugu yangu Makamu wangu(Tundu Lissu) anasema anahutubia taifa, ni Makamu Mwenyekiti (wa CHADEMA Bara) anahutubia taifa ameshakuwa kiongozi wa chama anahutubia taifa ni kukosa nidhamu. Sio Mwenyekiti wa chama soma katiba ya chama imeeleza kazi za Mwenyekiti na kazi za Makamu Mwenyekiti kila mmoja amefafanuliwa kwenye katiba kazi zake ni zipi anazifanyaje kama umeweza kwenda kufanya kazi ambayo si ya kwako.”

“Kama navyosema sio kila wakati kuchukua hatua ndiyo kumrekebisha kiongozi…sio kwamba hatumuelezi na hajui lakini mtu anapoamua kutoka nje ya misingi kwa sababu anafikiri labda yeye ni mkubwa kuliko chama kwamba yeye anaweza akafanya chochote anachotaka muda utaongea. Muda utazungumza ni nani mwenye haki na ukweli utabaki kuwa ukweli.”

Mbowe alipoulizwa kwamba Lissu anafanya kwa umakusudi na yeye Mbowe hachukui hatua labda anahisi ni kwa nini Lissu anafanya hivyo anafanya hivyo Mbowe akajibu “hilo swali ungemuuliza yeye angekusaidia zaidi.”
Kadiri Mhe Mbowe anavyozidi kuongea
Ndivyo anavyozidi kuidhihirisha chuki yake dhidi ya Lissu ..

Mwaka huu mlango ni wazi wagombea wa CCM.
Njia nyeupeee ..
 
1. Kwanza hakuna kanuni au kifungu ndani ya miongozo ya CHADEMA inayozuia mwanachadema yeyote kuongea na Watanzania wote.

2. Pili kila mtanzania ana haki ya freedom of speech inayompa haki ya kuongea na Watanzania wote.

3. Tatu, Lissu hakuongea na Watanzania ili kutoa msimamo wowote wa chama bali ameongea ya kwake anayotaka yeye, na wala hakuongea kwa kofia ya makamu mwenyekiti.

4. Mbowe aache kuongea kijumlajumla, aseme ni kanuni gani ya chama Lissu kakosea. Mwanasheria wa chama anaweza.kusaidia ktk hili.

5. Mbowe asitake kuwa mfalme wa chama, kwamba Yeye peke yake ndo mwenye haki ya kuongea waliobaki wans jukumu la kusikiliza tu. Natambua kuwa Mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa chama, hii haimaanishi kuwa eanschadema waliobaki ni mabubu.
 
Back
Top Bottom