Nowonmai
JF-Expert Member
- Jan 15, 2019
- 1,050
- 1,126
Chama cha siasa cha wakati huu kinagawanyika katika sehemu kuu tatu.
• Chama ndani ya wapiga kura.
• Chama kama oganaizesheni.
•Chama katika dola.
Kwa uchache tu, hapo awali, chama kinatakiwa kuwa na uwepo imara na wa kudumu kati ya wapiga kura kwa sababu kama chama kisipojipatia ushindi kwenye sanduku la kura katika ngazi husika mf udiwani, ubunge na urais, kitapotea mazima.
Chama kama oganaizesheni katika ngazi za kata, halmashauri, majimbo na kitaifa kinatakiwa kuunda au kuasili falsafa, itikadi, sera na kanuni za kukitambulisha, kuunganisha na kuongoza wanachama wake na wengine wanaovutiwa na siasa zake. Pia kujenga na
kusimamia miundo mbalimbali ya chama zikiwepo fedha, rasilimali watu, na miundombinu.
Chama katika dola ni pale ambapo kimepata ridhaa ya wananchi katika sanduku la kura kwa ngazi ya kuongoza serikali kuu, halmashauri, au hata uwakilishi tu mf udiwani au ubunge.
Hapa cha muhimu sana ni kuwa chama hicho kijikite kufikia malengo yake yaliyoanishwa kama ahadi kwa wapiga kura.
Mkuu mleta mada, na
kubaliana nawe kuwa ndani ya chama hicho na vingine vyote elimu inahitajika sana na wala sio kwa wanachama walei tu bali hata viongozi.
Elimu hiyo pia ikiwahusisha wananchi wote huenda tukapiga hatua walau moja mbele.
Inauma kusema hili lakini watanzania tumechelewa sana!