BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akizungumza kutoka Berlin Ujerumani, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema kwa mujibu wa Masharti ya Mkataba huo yanaonesha kuwa endapo kutakuwa na ulazima wa kuvunja Mkataba itabidi uamuzi utolewe na Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa.
Amesema DP World wanataka kupata haki ya kuendeleza, kuendesha na kuboresha Bandari zote za Baharini na Maziwa yote, kitu ambacho ni hatari kumwachia mtu mmoja kuhodhi hayo muhimu. Hali hiyo inaonesha Serikali haijapata funzo ilipobinafsisha TANESCO, TRL, ATCL na mashirika mengine.
Aidha, ameongeza Mkataba umeanza kutekelezwa kwa shughuli za awali baada ya kusainiwa wakati Bunge halijaupitia na kuridhia, hivyo Bunge linatumika kwasasa kwenda kupitisha tu na halina mamlaka ya kubadili chochote.