Pamoja na kwamba tupo msibani kuomboleza kifo cha mwanaAfrika na Mwanamajumui Hayati John Pombe Magufuli, imenilazimu kuhoji huyu ndiye Mh Lisu Wakili msomi aliyetaka kuwa Rais wetu 2020?
Nimesoma Twitter zake na maandiko yake mbalimbali baada ya msiba wa JPM. Nikajiuliza hivi huyu ndiye alipaswa kuwa Rais? Kwa tamaduni, mila na desturi za kitanzania na Afrika kwa ujumla si sawa kushangilia kifo hata Kama mtu alikuwa humpendi kwa kiwango chochote. Haturuhusu kumhukumu Marehemu, Mungu ndiye mwenye uwezo huo.
Tusiandike kama hatujawahi kufiwa au Kama sisi hatutakufa. Kila mtu duniani atakufa na atakufa kwa stahili yake. Kipindi hiki ambacho ndugu jamaa na rafiki wanapopitia kipindi kigumu sisi sote tunapaswa kuwafariji kwa kuwa hakuna anayejua kesho yake.
Nimpongeze Mh Mbowe ambaye statement yake inaonesha namna alivyoiva na anavyothamini uhai. Mh Mbowe ameonyesha nguvu yake ya maarifa na uhodari wa kuchambua maneno kulingana na mkutadha. Kwa mazingira haya simuoni mtu wa kuvaa viatu vya Mh Mbowe Kama mh Lisu ambaye nilidhani ni matured naye anaweza kuandika vitu vya kitoto ambavyo walau vingeandikwa na BAVICHA.
Tunatambua Lisu alipigwa na kuumizwa, lakini tunamshukuru Mungu mwingi wa rehema alimponya na sasa yupo hai, lakini kitendo cha kupona kwake hakiondoi ubinadamu na kupandikiza umbumbumbu kwenye argument na reasoning.
Lakini pia hii ni indicator kwenu CHADEMA Kama munadhani Lissu will be a good candidate for 2025, basi aingie darasani kwa mzee Mbowe kujifunza hekima na kuchambua mambo kabla ya pablicity.