Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 28,259
- 41,416
Njia pekee ni pressure tuuu huyu bibi atasusa na kujiondokea. Mapinduzi au mbinu yoyote ya aina yake haifai hata kidogo kwa nchi tuliyochagua kujitawala kidemokrasia na amani.Msingi wa hoja hii unajengwa na Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Toleo la mwaka 2005 kama ilivyonukuliwa hapa chini:-
8. (1). Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo:-
(a) Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi Kwa mujibu wa katiba hii;
(b) Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;
(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;
(d) Wananchi watashiriki katika shughuli za serikali yao Kwa mujibu wa masharti ya katiba hii
========================================
Kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya katiba hii, kumbe kila kiongozi mwenye madaraka na mamlaka ya kiserikali akiwemo aitwaye "Rais" amepewa au tumempa sisi wananchi.......
Kama ni hivyo, kumbe pia wakati wowote (si lazima kusubiri uchaguzi) tukiona hawezi au ameshindwa au anayatumia vibaya madaraka na mamlaka hayo, SISI TENA WANANCHI tunaweza kumtoa kwa njia halali kwa mujibu wa katiba hii hii katika muktadha wa Ibara hiyo hiyo ya 8 [1] (a) - (c) kwa kutumia njia halali 3 zifuatazo:
1. Shinikizo la umma (public pressure):
Hufanyika kwa utaratibu wa kupaza sauti kuonesha na kulisema tatizo. Sauti ikishindwa kusikika na kueleweka kwa wahusika, njia hii huenda hatua inayofuata ya juu zaidi yaani maandamano ya amani (mass mobilization) yakiwa yamebaba ajenda hiyo hiyo tu....
Hii njia ni very effective yenye kuleta matokeo ya haraka. Viongozi walengwa wanaiogopa sana. Na kwa sababu hii, njia hii mara zote huwa ni ngumu yenye risks nyingi kwa sababu huhusisha mapambano na vyombo vya dola kama polisi na hata Majeshi ya ulinzi ambayo huwa chini ya udhibiti na amri za kiongozi (Rais) anayekataliwa na kutakiwa kuondoka....
2. Kwa njia ya mashitaka ya ki - Bunge kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na wabunge maarufu kwa kiingereza kama "impeachment......"
Hii ni njia ngumu na pengine isiyowezekana kabisa ingalau katika mazingira ya sasa kwa sababu ya masharti yake kama yalivyo katika Katiba ya JMT Ibara ya 46A (1) - (11) sambamba na Ibara ya 90 (1) - (2) juu ya nguvu Rais aliyonayo kulivunja Bunge wakati wowote kwa sababu anayoweza hata kuitengeneza tu......
3. Kwa njia ya uchaguzi wa HAKI, HURU na wa WAZI.
Hii ndiyo njia kuu ya kidemokrasia iwapo mambo yako kawaida. Chaguzi mara nyingi zina vipindi vya muda maalumu. Hapa kwetu Tanganyika ni kila baada ya miaka mitano....
Kwa mazingira ya Rais aliyeshindwa kutekeleza wajibu wake, wananchi na nchi haiwezi kusubiri miaka mitano ifike ndiyo tuondoe tatizo......
##Ndo kusema kuwa movement ya CHADEMA ya "SAMIA MUST GO" si kuvunja kuvunja wala sheria yoyote ile. Hili ni shinikizo la umma kwa mtu ambaye yuko chini ya mamlaka yao kushindwa kutekeleza wajibu wake kwa makusudi au kwa kuwa tu uwezo kiuongozi ni mdogo.....
##Polisi wao ndiyo wanavunja sheria na Katiba kwa kuanza kutisha watu ili wasi - exercise haki yao kuwajijibisha kiongozi wao (Rais) ambaye ame - prove total failure ktk kulinda uhai wa wananchi/watulioshindwa kwa mujibu wa Ibara ya 8 [1] (a) - (c)...
##Katika hali hii, wananchi (umma) ni lazima tuyatumie mamlaka yetu kwa ukamilifu...!
Muhimu ni hiyo political pressure bi hangaya asusie mkate kwa amani au 2025 tumdondoshe kwenye sanduku la kura!