Pre GE2025 Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
apoo sasa angalau wanaonekana maana tulianza kuzan wanaogopa na wamenyosha mikono bt she must GO
 
Wenye "Ruto Must Go" hawakufanikiwa ndiyo waje kufanikiwa watanzania? Watanzania wakiamzisha hiyo ya "Samia Must Go" dunia nzima itajua wanafanya maigizo ili wapate viewers mitandaoni.
Miaka hii ni nadra sana kwa nafasi kujirudia mara mbili. Walipoitisha Opareshini Ukuta kipindi kile cha Magufuli, wanamchi waliitika sana, Mbowe akafanya kosa kubwa sana la kusimamisha maandamano yale kisa viongozi wa dini walimwita na kumtaka ayasitishe na kwamba kama ana madai wao watayapeleka kwa rais.
Mara ya pili ni hapo juzi kwenye maziko ya Ally Kibao kule Tanga, Public ilishapata joto la asili, yeye akaleta busara zisizo na lazima akapooza joto lile pasipo sababu. Hilo ni kosa kubwa sana.
Pamoja na uzuri wake, hakuna jambo atalifanya Mbowe katika siasa za sasa likafanikiwa. Simshauri maamuzi gani afanye, bali namshauri asome na kupuma alama za nyakati. Siasa za hivi sasa hazihitaji busara ndiyo maana CCM na serikali hawasiti kuua yeyote pale inapohitajika
 
Mbowe ni mtu mwema na hataki damu imwagike. Angekuwa na akili kama zenu CHADEMA kingeshakufa
 
Huu ni uamuzi sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…