Dunia ya Mungu ina mengi. Ndiyo maana waungwana walisema ukiyastaajabu ya Mussa jiandae kuyaona ya Firauni.
Inasemekana Freeman Aikaeli Mbowe alikuwa mtoto wa ubatizo kwa hayati baba wa taifa ambaye ndiye aliyempa jina Freeman, akimhusisha na siku aliyobatizwa:
Kwamba pia Makongoro Nyerere alikuwa mtoto wa ubatizo kwa baba yake Mbowe.
Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja nyuma.
Kua uyaone.
Miaka 60 baadaye yatima huyu mwenye malezi yenye mafungamano na pande za Magogoni amegeuzwa leo kuwa gaidi hatari wa kiwango cha akina Osama bin Laden na serikali ya mheshimiwa SSH:
Yote hii ikiwa ni fitina na figisu za kisiasa zitokanazo na yeye kupanga kushiriki kongamano la kudai katiba mpya, jambo ambalo si kosa kwa mujibu wa katiba.
Imefanana sana na yule mwenye shamba la mizabibu aliyelazimika hatimaye kumtuma mwanawe kwenda kuchukua sehemu ya yaliyokuwa mazao yao (Mathayo 21:33-46):
"Lakini wale wakulima walipomwona mwanawe wakasemezana wao kwa wao: ‘Huyu ndiye mrithi; na tumuue ili tuuchukue urithi wake!’ Basi, wakamkamata, wakamtoa nje ya lile shamba la mizabibu, wakamuua."
Eh Mola wetu na ukamsimamie Freeman Aikaeli Mbowe kokote kule aliko ukiwalipa wote walio watesi wake, sawa sawa na matendo yao.