Alpaslan Bey
Senior Member
- Nov 4, 2023
- 121
- 163
Nimeona mh Mbowe akitaja fadhila ambazo amemfadhili mh Tundu Lissu tangu walipokutana mwaka 1995 na kuamua kushirikiana naye katika harakati za kisiasa nchini.
Wahenga wanasema, "tenda wema uende zako" na sio kusubiri fadhila. Mwl Nyerere aliwahi kupewa nyumba ya kuishi na marehemu Dosa Azizi na gari alilokuwa akitumia mara nyingi kwenye harakati za ukombozi lilikuwa la ndg Dosa Azizi lakini cha kushangaza baada ya kufanikiwa kuupata uhuru wetu kutoka kwa mwingereza, Dosa hakupewa hata ukuu wa wilaya na bado aliendelea kuwa mtulivu pasipo kuonyesha manung'uniko ya aina yoyote.
Dosa hakukumbuka chakula chake alichokuwa anailisha familia ya Nyerere, hakukumbuka nyumba yake, hakukumbuka gari lake, mafuta yake na muda wake aliotumia kwa ajili ya kumfadhili Nyerere na garakati za uhuru.
Naamini kama Mbowe angekubali ushauri na kusoma alama za nyakati angeweza kulinda heshima yake aliyojijengea muda mrefu.
Uamuzi wa kuendelea kugombea ndio uliofanya leo anayaongea haya mambo ya fadhila jambo linalopelekea wengine kuona kama amefilisika kisiasa. Kama uliamua kumfadhili mtu kuna haja gani ya kuongea hadharani? na. Kwa nini iwe leo na sio wakati huo ambao huo ufadhili ulitolewa? Kwa tusiamini umefikia hatua hiyo baada ya aliyefadhiliwa kutishia maslahi yako kwa kuchukua fomu ili mshindane??
Wanasiasa wa leo tuna kila sababu ya kujifunza kwa waasisi wetu kama kina Dosa Azizi ili kujiepusha na vinyongo, visasi na mshangao ikiwa mambo yatakwenda tofauti.