Mocumentary
JF-Expert Member
- Jul 31, 2017
- 806
- 2,049
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe wakati akiongea na Diaspora nchini Marekani leo amesema anakasirishwa na wanaosema amelamba asali ili kumfanya akae kimya, na kusema hilo ni kama tusi kwake lakini anavumulia kwakuwa ni sehemu ya harakati.
"Nimekuwa nikifuatilia mijadala katika mitandao, hisia za Viongozi wenzangu ndani ya Chama, hisia za Watanzania wengine wasio Wana CHADEMA, wengi wakiamini kwamba maridhiano (Kati ya CHADEMA na Serikali) ni kupoteza muda, na hapo katikati ukatokea msamiati kuwa Mbowe kalamba asali, mbona Mbowe hazungumzi, Mbowe amekuwa kimya sana"
"Naomba leo niweke rekodi sawa, Chama ninachokiongoza nimekiruhusu sana kusema wala sitaki kiwe Chama ambacho akizungumza Mwenyekiti basi wenzake wote wakae kimya, hapana"
"Kwanza katoka Makamu wangu Lissu akazungumza, ukimsikia Lissu kasema ukiangalia kwa haraka unaweza kufikiria Mbowe na Lissu wana ugomvi lakini huyu ni Mtu amepigwa risasi 16 hawa ni Viongozi wenzangu wamefungwa Jela, wanaishi ughaibuni kwa kulazimishwa, ni lazima uelewe hisia na uchungu wao, hii ya 'Mbowe kalamba asali' inaniudhi lakini inabidi nikubali, nikasema OK, kama kulamba asali ni kuitetea Nchi yangu niko tayari kuitetea"
"Nimekuwa kwenye upinzani kwa miaka 30, sio kwa kuangalia madaraka wala fedha bali mustakabali wa Tanzania, nimepoteza vitu vingi, hiyo asali nitakayopewa leo inaweza kufidia miaka yangu 30 ya jasho na maumivu?, ni tusi lakini tunaikubali kwasababu ni sehemu ya harakati"
Soma hoja hizi:
1) Mbowe kauza utu wake. Hakutakiwa kukubali kulamba asali kirahisi namna hii
2) Pamoja na kulamba Asali, Mbowe alaani utitiri wa magari, msafara wa Rais hauendani na kubana matumizi
3) WanaCHADEMA wengi hatupendi namna Mbowe alivyolamba asali ila hatuna namna maana hatuna maamuzi
4) Mama Samia asali uliyompimia Mbowe muongezee kidogo maana naona kama imepungua akikuzingua mpe Alovera
5) Wapo wapi watetezi wa Watanzania, wamesusa au wanalamba asali?