Kwa uelewa wangu Dhana ya kulamba asali tafsiri yake ni kwamba, walio na mamlaka wanayatumia vibaya kwa kujinufaisha wao zaidi na kuwakandamiza wasio na mamlaka. Yaani hawatendi haki.
Dhana ya kulambishwa asali,ni pale Anapotokea mpinzani wao anayewafungua macho watu, ndipo inabidi wenye mamlaka wampatie fursa ya kunufaika na yeye,ili kumstopisha asiendelee kuwapigania wanyonge wenzake.
Katika muktadha huo yupi ni hatari zaidi kwetu mlamba asali ambaye pia ni mlambisha asali au mlambishwa asali?
Tuanzie hapo.