Mbowe ndiye anayewafanya Wajinga na siyo Spika Tulia au CCM!

Mbowe ndiye anayewafanya Wajinga na siyo Spika Tulia au CCM!

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Sijui ni kitu gani kinawafanya muone Mbowe jinsi mnavyomuona kwamba ni Malaika, sasa mnaamini kabisa ule Mkutano Mlimani ulikuwa real ? Kwa nini hamuulizi maswali ?

Iweje waliofukuzwa Ubunge warudi Bungeni wakati Mbowe yuko karibu sana na Raisi Samia na hata anakwenda kumtembelea muda wowote Ikulu akiamua?

Kama ni kweli Mbowe au sijui ni baraza la chadema alinuia kuwafukuza akina Halima Mdee kwa nini warudi Bungeni bila consequences zozote ?

Aidha Mbowe amewaloga na mnashindwa kuona lolote baya analowafanyia ?

1652427928188.jpeg
 
Kama chadema wameisha peleka barua rasmi bungeni juu ya maamuzi yao ya kuwafukuza wale wabunge 19 uanachama...basi ni SPIKA ndie anawafanya Watanzania WAJINGA sio Mbowe....nguvu ya Mbowe na Chadema kuwazuia wale wabunge wasitinge Bungeni iliishia pale Mlimani City kwenye baraza kuu...na ilichobaki ni Kiongozi wa bunge kutimiza wajibu wake pindi tu akipokea taarifa rasmi ya uamuzi ule...lakini kama taarifa ya kufukuzwa uanachama haijamfikia basi wale bado ni wabunge na niwajibu wa Spika kulinda Ubunge wao...
 
Kile kitendo cha kubadili ule msimamo wao mkali wa kutojihusisha na kuchangamana na wabunge au viongozi waliopatikana kutokana na uchaguzi 2020 ambao waliutambua kama batili, na ile ya mbowe kusema hawezi kwenda ikulu pekeake kama anakwenda kuchumbia kisha ghalfa akaenda huku akitabasamu, ilipaswa kuwashitua kwenye usingizi wao mzito.

Hili sakata la wabunge litawasumbua hivihivi mpaka huu mhula wa kiuongozi unaisha.
 
Ni wazi haya anayoyafanya Spika kuhusu akina Halima Ni delaying tactics. Hiyo kesi kamwe haitaisha mpàka 2025.

The only solution Ni Mwenyekiti Freeman Mbowe kumuona Samia kuhusu upuuzi huu wa Tulia na Ni deliberate move to block justice na kuiweka Chadema katika mgogoro.

Short of that Ni ubatili mtupu na huo mkutano wenu msipoteze muda maana majibu ya Samia kuhusu hili la akina Mdee yana predict future trend!
 
Wewe si unamsifia Samia kuwa anaupiga mwingi-kiko wapi?!
 
Ajabu sana, Spika anasema wakina Mdee wameenda mahakamani kudai uanachama wao waliofukuzwa Chadema.

Sasa kama Spika anakiri wakina Mdee hawana chama wanachokiwakilisha bungeni, kule bungeni wapo wanafanya nini?

Hapa ni wazi kuna mchezo unaochezwa kati ya CCM na hizi taasisi zake, nasisitiza Mbowe ajitafakari na chama chake kuhusu umuhimu wa vile vikao vya maridhiano wanavyofanya ikulu.

Binafsi sioni umuhimu wa kukutana na watu wanaoendelea kuvunja sheria mbele ya macho yenu, hizi ni dharau.
 
Hizi pilika zote za namna ya kuwalinda hao wasaliti ,Rais Samia ameshakuwa informed, Rais Samia hataki maridhiano, Rais Samia hajiamini na ni muoga sana akiifikiria 2025.

So, CDM wala wasihangaike tena na huyo Mama ni mnafiki na ni mtu anayepelekeshwa pelekeshwa na wenye system.

Hakuna mahala maridhiano na shetani yakafanikiwa, NEVER.!
 
Mnataka Mheshimiwa Rais aingilie Mhimili mwingine, and you still call yourselves democratic!
Hapa sio suala la kuingilia mhimili mwingine. ni kuangalia sheria zilizopo zinasema nini kuhusu wakina Mdee na wenzake mpaka muda huu.

Katiba inatamka wazi, kifungu cha 67 (1) (b) wabunge lazima wawe wanatokana na chama cha siasa ili wahalalishe uwepo wao bungeni, tofauti na wale wanaoteuliwa na Rais.

Wale kina Mdee wamefukuzwa uanachama, maana yake kule bungeni mpaka muda huu hawatokani na chama chochote, hawa wanavunja sheria kwa uwepo wao bungeni.

Spika Tulia ni mwanasheria, ina maana haoni huu uvunjifu wa sheria anaousimamia tena akiwa kama kiongozi wa chombo cha kutunga sheria? hizi ni dharau kwa watanzania.
 
Kinacholeta ugumu hapo ni kua wakiwatoa covid 19, bunge litabaki halina upinzani litakua bunge la chama kimoja, tutakosa misaada ya wahisani, hapo ndo mtaona kua uchaguzi wa 2020 jiwe lilifanya mambo ya kijinga bila kujifikilia,

cha msingi hapo chadema wakubali kama wanawatoa covid 19 basi walete majina mengine ili walau bungeni kuwemo na vyama viwili
 
Hapa sio suala la kuingilia mhimili mwingine. ni kuangalia sheria zilizopo zinasema nini kuhusu wakina Mdee na wenzake mpaka muda huu.

Katiba inatamka wazi, wabunge lazima wawe wanatokana na chama cha siasa ili wahalalishe uwepo wao bungeni.

Wale kina Mdee wamefukuzwa uanachama, maana yake kule bungeni mpaka muda huu hawatokani na chama chochote, hawa wanavunja sheria kwa uwepo wao bungeni.

Spika Tulia ni mwanasheria, ina maana haoni huu uvunjifu wa sheria anaousimamia tena akiwa kama kiongozi wa chombo cha kutunga sheria? hizi ni dharau kwa watanzania.
Hizo sheria zitaenda kuangaliwa mahakamani.

Anachotaka mwanzilishi wa huu uzi ni Mheshimiwa Rais kuingilia mhimili huru wa mahakama in favour of CHADEMA.

Does anything justify this barbarism?
 
Ni wazi haya anayoyafanya Spika kuhusu akina Halima Ni delaying tactics. Hiyo kesi kamwe haitaisha mpàka 2025.
The only solution Ni Mwenyekiti Freeman Mbowe kumuona Samia kuhusu upuuzi huu wa Tulia na Ni deliberate move to block justice na kuiweka Chadema katika mgogoro. Short of that Ni ubatili mtupu na huo mkutano wenu msipoteze muda maana majibu ya Samia kuhusu hili la akina Mdee yana predict future trend!
Ya nini yote hayo? Chadema imeshafanya wajibu wake, mengine wawaachie Wananchi wanaona. Sioni sababu ya kuanza kufuatilia wametoka au hawajatolewa. Tunawasubiri tuone watatuambia Nini na hizi double standard zào.
 
Mnataka Mheshimiwa Rais aingilie Mhimili mwingine, and you still call yourselves democratic!
Well maybe you are right. But how many times rais ameingilia maamuzi ya mihimili mingine?
Starting with awamu zilizopita?

In Tz rais akiamua hata kama ni jambo la muhimili flani hakuna wa ku object. and hiyo ndio weakness ya mifumo yetu
 
Mbowe na wenzie wasijidanganye kuwa watapewa katiba na tume mpya kwa njia za amani. Hili halijawezekana tangu 1992 mfumo wa chama kimoja ulipoanza. Halitawezekana hadi mwisho. CCM wanajua wanavyo "shinda" chaguzi. Hawawezi kukubali mfumo wa haki. Inabidi walazimishwe. Mbowe bado hajalijua hilo. Atasubiri sana hadi atastaafu siasa.
Hizi pilika zote za namna ya kuwalinda hao wasaliti ,Rais Samia ameshakuwa informed, Rais Samia hataki maridhiano, Rais Samia hajiamini na ni muoga sana akiifikiria 2025.

So, CDM wala wasihangaike tena na huyo Mama ni mnafiki na ni mtu anayepelekeshwa pelekeshwa na wenye system.

Hakuna mahala maridhiano na shetani yakafanikiwa, NEVER.!
 
Mbowe alifuata nini Ikulu tena peke yake na yakiwa yamebaki masaa machache kikao kilichowafukuza kina Mdee kufanyika?!

Ni kweli Mbowe hana maslahi ya uwepo wa kina Mdee huko Bungeni?!
 
Ni wazi haya anayoyafanya Spika kuhusu akina Halima Ni delaying tactics. Hiyo kesi kamwe haitaisha mpàka 2025.
The only solution Ni Mwenyekiti Freeman Mbowe kumuona Samia kuhusu upuuzi huu wa Tulia na Ni deliberate move to block justice na kuiweka Chadema katika mgogoro. Short of that Ni ubatili mtupu na huo mkutano wenu msipoteze muda maana majibu ya Samia kuhusu hili la akina Mdee yana predict future trend!

Ndiyo mchezo wa Siasa huo, rejea kesi ya Zitto Kabwe miaka ile. Na kama hawakuwapa nafasi ya kusikilizwa kujieleza wakakimbilia kupiga kura tu basi majamaa hawa lazima washinde bila kupepesa macho. Rejea hukumu ya akina Sabaya hivi karibuni ambapo ilifutwa miaka 30 hadi 0 kwa sababu washitakiwa watatu hawakupewa haki ya kusikilizwa. Hii itacheza hadi miezi ya Agosti 2025. Baada ya hapo majamaa yatavuta kilicho chao na kuhamia vyama vingine, na hapo mchezo utakuwa umeisha!
 
Well maybe you are right. But how many times rais ameingilia maamuzi ya mihimili mingine?
Starting with awamu zilizopita?

In Tz rais akiamua hata kama ni jambo la muhimili flani hakuna wa ku object. and hiyo ndio weakness ya mifumo yetu
Do two wrongs make a right?
 
Back
Top Bottom