Mbowe: Niliona John Heche anapotea kisiasa, nikamteua Mjumbe wa Kamati Kuu

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2018
Posts
882
Reaction score
3,337
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema aliamua kumteua John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ili kumuepusha na hatari ya kupotea kwenye siasa za juu za chama.

Mbowe aemetoa kauli hiyo jana, Januari 17, 2025, wakati wa mahojiano maalum na wahariri na waandishi wa habari kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema kuwa, nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na viongozi wenye nguvu na uwezo wa kulijenga.

Pia amebainisha kuwa Heche, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu, alishindwa kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa na Esther Matiko katika uchaguzi wa kanda.

“Nikaona kwamba mtu huyu atapotea kwenye siasa za juu za chama. Kwa hiyo, Heche ndiye mtu pekee niliyemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka mitano ambayo sasa inakaribia kuisha,” alisema Mbowe.

Kwa mujibu wa Mbowe, Katiba ya CHADEMA inampa Mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa Kamati Kuu, nafasi ambazo mara nyingi huzijaza kwa uangalifu mkubwa.

Sambamba na hilo, Mbowe ameeleza kuwa alimuheshimu Heche kwa mchango wake na hivyo alimchagua tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano wakati chama kilipokuwa kinashiriki mchakato wa maridhiano.

“Tulivyokuwa tunaenda kwenye maridhiano, Kamati Kuu ilinipa jukumu la kuchagua wajumbe wa kwenda nao, nikamchagua tena Heche,” alisema.

Hata hivyo, Mbowe ameelezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Heche kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa maridhiano.

Miongoni mwa madai hayo ni kwamba wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikuwa wakilipwa Shilingi milioni tatu kwa kila kikao, madai ambayo yalikanushwa.

“Tulivyombana kuhusu kauli hiyo, Heche alisema alikuwa anatania tu. Lakini shutuma kama hizo ni za uongo na zinaweza kudhoofisha imani ya wanachama na umma kwa ujumla,” aliongeza Mbowe.

Mbowe alihitimisha kwa kusisitiza kuwa uongozi ndani ya chama unapaswa kuzingatia ukweli, mshikamano, na nidhamu, akionyesha dhamira yake ya kuendelea kulijenga chama kwa kushirikiana na viongozi wote.

Jambo TV
 
Heche tumsamehe, kaingia katika kundi ambako silo bila kujua athali zake binafsi za kisiasa.
Siasa za chuki, kudhalilishana, kusengenyana hazina afya kwa chama. Wajumbe tusaidieni genge hili likataeni kwa kauli moja kama tulivyoukataa ugonjwa wa ukoma miaka ile ya 70.
 
Leo na wewe ni chadema tena wa kumtetea mbowe kbs wewe huyu huyu fuso sjui canter umekuwa mwanachadema ni kwamba maccm hamtaweza kamwe kutuchagulia mwenyekt wa chama mwenye mahaba na mwenyekt wa majizi ya taifa hli maccm
 
Hatuwezi kuwapa chama watu wa fitna ambao hawathamini kazi walizofanya wenzao hadi chama kikafikia hapo kilipo.

NIDHAMU ndiyo inakwenda kummaliza Lissu kesho kutwa.
Sasa ataamua mwenyewe kubakia ama kuondoka, ila tunamshauri abaki ajirekebishe na ashiriki kuijenga CDM baada ya uhalibifu mkubwa alioufanya yeye wa genge lake.
 
Katika wapiga debe wa Lissu, ni Heche peke yake ndiye amekuwa akimpa heshima zake Mbowe. Pamoja na kumtaka apumzike, amekataa kumpaka matope. Amesema pia kwa uwazi tu kuwa mchango wa Mbowe ni muhimu na bado unahitajika. Ameonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Mimi ningependa awe Makamu Mwenyekiti chini ya Mbowe ili 2030 agombee uenyekiti.
Bahati mbaya Wenje amechafuliwa mno na hana charisma ya Heche.
Kumchagua Heche na Mbowe kutakuwa hatua ya kwanza ya kutibu majeraha ya kampeni hii maana kila upande utakuwa na mtu wake. Alternative ya Lissu na Wenje haiwezi kufanya kazi vizuri kwa pamoja.

Amandla....
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema aliamua kumteua John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ili kumuepusha na hatari ya kupotea kwenye siasa za juu za chama.

Mbowe aemetoa kauli hiyo jana, Januari 17, 2025, wakati wa mahojiano maalum na wahariri na waandishi wa habari kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema kuwa, nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na viongozi wenye nguvu na uwezo wa kulijenga.

Pia amebainisha kuwa Heche, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu, alishindwa kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa na Esther Matiko katika uchaguzi wa kanda.

“Nikaona kwamba mtu huyu atapotea kwenye siasa za juu za chama. Kwa hiyo, Heche ndiye mtu pekee niliyemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka mitano ambayo sasa inakaribia kuisha,” alisema Mbowe.

Kwa mujibu wa Mbowe, Katiba ya CHADEMA inampa Mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa Kamati Kuu, nafasi ambazo mara nyingi huzijaza kwa uangalifu mkubwa.

Sambamba na hilo, Mbowe ameeleza kuwa alimuheshimu Heche kwa mchango wake na hivyo alimchagua tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano wakati chama kilipokuwa kinashiriki mchakato wa maridhiano.

“Tulivyokuwa tunaenda kwenye maridhiano, Kamati Kuu ilinipa jukumu la kuchagua wajumbe wa kwenda nao, nikamchagua tena Heche,” alisema.

Hata hivyo, Mbowe ameelezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Heche kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa maridhiano.

Miongoni mwa madai hayo ni kwamba wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikuwa wakilipwa Shilingi milioni tatu kwa kila kikao, madai ambayo yalikanushwa.

“Tulivyombana kuhusu kauli hiyo, Heche alisema alikuwa anatania tu. Lakini shutuma kama hizo ni za uongo na zinaweza kudhoofisha imani ya wanachama na umma kwa ujumla,” aliongeza Mbowe.

Mbowe alihitimisha kwa kusisitiza kuwa uongozi ndani ya chama unapaswa kuzingatia ukweli, mshikamano, na nidhamu, akionyesha dhamira yake ya kuendelea kulijenga chama kwa kushirikiana na viongozi wote.

Jambo TV
Yeriko Nyerere ameonesha ukomavu katika kumkingia kifua Mwamba, mbona hamumsifii huyu? 😆 😆 😆 😆
 
Sasa hayo si mambo ya kawaida tu kwa mujibu wa katiba yenu. Yanauhusiano gani na uchaguzi huu. Kwani hata Lissu akishinda anaweza kukuteua mbowe uwe mjumbe wa hiyo kamati.
 
Mbowe amekosa hoja kiasi hicho? Yaani akifanya majukumu yake anataka watu wasigombee nafasi zinazotakiwa kujazwa? Mbona amekosa hoja kama mwenyekiti wa upande wa pili anaeongoza kikao leo...yaani kujiamini zero kabisa.
 
Ana maanisha ajijenge na akijenge chama kwnz..
 
Mbowe amekosa hoja kiasi hicho? Yaani akifanya majukumu yake anataka watu wasigombee nafasi zinazotakiwa kujazwa? Mbona amekosa hoja kama mwenyekiti wa upande wa pili anaeongoza kikao leo...yaani kujiamini zero kabisa.
Hoja muhimu FAM anamtaka Heche ajijenge na akijenge chama..kulikoni hiki anachoafanya
 
Kwa hiyo alimhonga nafasi ya ujumbe wa kamati kuu ili siku zote awe anamuunga mkono pindi akitaka kugombea uenyekiti au?
Kwa nini ukimbilie ni hongo usione alimuona atafika mbali yanii Maono...anamtaka kijana awe nidhamu huku vile vile ajijenge kisiasa ndani ya chama
 
Katika wapiga debe wa Lissu, ni Heche peke yake ndiye amekuwa akimpa heshima zake Mbowe. Pamoja na kumtaka apumzike, amekataa kumpaka matope. Amesema pia kwa uwazi tu kuwa mchango wa Mbowe ni muhimu na bado unahitajika. Ameonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Mimi ningependa awe Makamu Mwenyekiti chini ya Mbowe ili 2030 agombee uenyekiti.
Bahati mbaya Wenje amechafuliwa mno na hana charisma ya Heche.
Kumchagua Heche na Mbowe kutakuwa hatua ya kwanza ya kutibu majeraha ya kampeni hii maana kila upande utakuwa na mtu wake. Alternative ya Lissu na Wenje haiwezi kufanya kazi vizuri kwa pamoja.

Amandla....
Lakini MBOWE anasema HECHE anamtukana.
 
Back
Top Bottom