Mbowe: Niliona John Heche anapotea kisiasa, nikamteua Mjumbe wa Kamati Kuu

Mbowe: Niliona John Heche anapotea kisiasa, nikamteua Mjumbe wa Kamati Kuu

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema aliamua kumteua John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ili kumuepusha na hatari ya kupotea kwenye siasa za juu za chama.

Mbowe aemetoa kauli hiyo jana, Januari 17, 2025, wakati wa mahojiano maalum na wahariri na waandishi wa habari kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam.

Mbowe amesema kuwa, nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na viongozi wenye nguvu na uwezo wa kulijenga.

Pia amebainisha kuwa Heche, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu, alishindwa kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa na Esther Matiko katika uchaguzi wa kanda.

“Nikaona kwamba mtu huyu atapotea kwenye siasa za juu za chama. Kwa hiyo, Heche ndiye mtu pekee niliyemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka mitano ambayo sasa inakaribia kuisha,” alisema Mbowe.

Kwa mujibu wa Mbowe, Katiba ya CHADEMA inampa Mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa Kamati Kuu, nafasi ambazo mara nyingi huzijaza kwa uangalifu mkubwa.

Sambamba na hilo, Mbowe ameeleza kuwa alimuheshimu Heche kwa mchango wake na hivyo alimchagua tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano wakati chama kilipokuwa kinashiriki mchakato wa maridhiano.

“Tulivyokuwa tunaenda kwenye maridhiano, Kamati Kuu ilinipa jukumu la kuchagua wajumbe wa kwenda nao, nikamchagua tena Heche,” alisema.

Hata hivyo, Mbowe ameelezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Heche kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa maridhiano.

Miongoni mwa madai hayo ni kwamba wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikuwa wakilipwa Shilingi milioni tatu kwa kila kikao, madai ambayo yalikanushwa.

“Tulivyombana kuhusu kauli hiyo, Heche alisema alikuwa anatania tu. Lakini shutuma kama hizo ni za uongo na zinaweza kudhoofisha imani ya wanachama na umma kwa ujumla,” aliongeza Mbowe.

Mbowe alihitimisha kwa kusisitiza kuwa uongozi ndani ya chama unapaswa kuzingatia ukweli, mshikamano, na nidhamu, akionyesha dhamira yake ya kuendelea kulijenga chama kwa kushirikiana na viongozi wote.

Jambo TV
Mbowe has a God complex.
 
Katika wapiga debe wa Lissu, ni Heche peke yake ndiye amekuwa akimpa heshima zake Mbowe. Pamoja na kumtaka apumzike, amekataa kumpaka matope. Amesema pia kwa uwazi tu kuwa mchango wa Mbowe ni muhimu na bado unahitajika. Ameonyesha ukomavu wa hali ya juu.
Mimi ningependa awe Makamu Mwenyekiti chini ya Mbowe ili 2030 agombee uenyekiti.
Bahati mbaya Wenje amechafuliwa mno na hana charisma ya Heche.
Kumchagua Heche na Mbowe kutakuwa hatua ya kwanza ya kutibu majeraha ya kampeni hii maana kila upande utakuwa na mtu wake. Alternative ya Lissu na Wenje haiwezi kufanya kazi vizuri kwa pamoja.

Amandla....
Umenena vyema, Heche bado ana nafasi kubwa ya kuwa makamo endapo atakili kwamba anaweza kufanya kazi na Mwamba ili baada ya miaka 3 tu tunampa uongozi mkuu wa chama.
Kwani ameonyesha heshima na kutambua mchango wa Mh mbowe.

Kumbuka uchaguzi ujao utawahi ili kutoendana na ratiba ya uchaguzi mkuu na ule wa serikali za mitaa.
 
Back
Top Bottom