johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Basi ndio sababu alitaka kumfanya Heche awe chawa wake 🐼Mbowe swala tano.Ustadhi Aboubari Mbowe ukipenda.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi ndio sababu alitaka kumfanya Heche awe chawa wake 🐼Mbowe swala tano.Ustadhi Aboubari Mbowe ukipenda.
Heche ni mhuni,hivi unajua alidanganya wanachama eti wanalamba 3 milioni per kikao kumbe walikuwa wanapokea 250,000 tu.Basi ndio sababu alitaka kumfanya Heche awe chawa wake 🐼
Anamzidi Mbowe kielimu 😂Heche ni mhuni,hivi unajua alidanganya wanachama eti wanalamba 3 milioni per kikao kumbe walikuwa wanapokea 250,000 tu.
Baada ya kubanwa kwanini anasema uongo akasema eti alikuwa anatania.
Kama elimu ni sababu basi maprofesor wangekuwa wakuu wa kila kitu.Anamzidi Mbowe kielimu 😂
Kila Kitu ndio nini Bwashee 😂Kama elimu ni sababu basi maprofesor wangekuwa wakuu wa kila kitu.
FAM anashinda tenaMwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, amesema aliamua kumteua John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho ili kumuepusha na hatari ya kupotea kwenye siasa za juu za chama.
Mbowe aemetoa kauli hiyo jana, Januari 17, 2025, wakati wa mahojiano maalum na wahariri na waandishi wa habari kutoka kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) jijini Dar es Salaam.
Mbowe amesema kuwa, nafasi yake kama Mwenyekiti wa chama ni kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na viongozi wenye nguvu na uwezo wa kulijenga.
Pia amebainisha kuwa Heche, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti na Mjumbe wa Kamati Kuu, alishindwa kurejea kwenye nafasi hiyo baada ya kushindwa na Esther Matiko katika uchaguzi wa kanda.
“Nikaona kwamba mtu huyu atapotea kwenye siasa za juu za chama. Kwa hiyo, Heche ndiye mtu pekee niliyemteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu kwa miaka mitano ambayo sasa inakaribia kuisha,” alisema Mbowe.
Kwa mujibu wa Mbowe, Katiba ya CHADEMA inampa Mwenyekiti nafasi ya kuteua wajumbe sita wa Kamati Kuu, nafasi ambazo mara nyingi huzijaza kwa uangalifu mkubwa.
Sambamba na hilo, Mbowe ameeleza kuwa alimuheshimu Heche kwa mchango wake na hivyo alimchagua tena kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maridhiano wakati chama kilipokuwa kinashiriki mchakato wa maridhiano.
“Tulivyokuwa tunaenda kwenye maridhiano, Kamati Kuu ilinipa jukumu la kuchagua wajumbe wa kwenda nao, nikamchagua tena Heche,” alisema.
Hata hivyo, Mbowe ameelezea masikitiko yake kuhusu hatua ya Heche kutoa taarifa za uongo kuhusu mchakato wa maridhiano.
Miongoni mwa madai hayo ni kwamba wajumbe wa Kamati ya Maridhiano walikuwa wakilipwa Shilingi milioni tatu kwa kila kikao, madai ambayo yalikanushwa.
“Tulivyombana kuhusu kauli hiyo, Heche alisema alikuwa anatania tu. Lakini shutuma kama hizo ni za uongo na zinaweza kudhoofisha imani ya wanachama na umma kwa ujumla,” aliongeza Mbowe.
Mbowe alihitimisha kwa kusisitiza kuwa uongozi ndani ya chama unapaswa kuzingatia ukweli, mshikamano, na nidhamu, akionyesha dhamira yake ya kuendelea kulijenga chama kwa kushirikiana na viongozi wote.
Jambo TV
Mbowe kila siku ni mtu wa nyuma ya pazia. Wakina Lissu na Lema walidanganyika na Club House. Kule wamejaa watu wa nadharia na sio watekelezaji. Na unfortunately hawaruhusu dissent...Mbowe angekuwa pro-active namna hii wakati wa maridhiano, chama kisingetumbukia ktk matatizo waliyonayo.
..pia wakati umefika kwa yeye kama mgombea kuunga mkono mabadiliko yote aliyoyapendekeza Tundu Lissu.
..Tundu Lissu anaweza kuwa wrong katika uwasilishaji wa hoja zake, lakini hajakosea ktk uhalali wa hoja hizo.
..Jambo lingine ni kuacha mizengwe. Kuna malalamiko mengi ya Mbowe kuumiza wenzake. Suala hili limejirudia sana, Mbowe ajirekebishe.
Amesema wapi kuwa Heche amemtukana? Mbona mnaleta uongo wa kijinga? Mbowe amesema kuwa Heche alisema uongo kuwa wanalipwa mamilioni wanapohudhuria vikao vya maridhiano. Alipobanwa, akasema alikuwa anatania. Na haya yalitokea kabla ya haya mambo ya sasa.Halafu kitu kibaya zaidi wafuasi wake wanasema Heche kaongea vizuri sana kwa kumuheshimisha yeye MWAMBA, lakini MWAMBA Mwenyewe anasema HECHE anamtukana.
Concept za Goebbels hazifanyi kazi hapa.Lakini MBOWE anasema HECHE anamtukana.
Mbowe kila siku ni mtu wa nyuma ya pazia. Wakina Lissu na Lema walidanganyika na Club House. Kule wamejaa watu wa nadharia na sio watekelezaji. Na unfortunately hawaruhusu dissent.
Akifanya hivyo itaonekana kama ka capitulate. Akishinda watajadili kwenye vikao maana watu wa Lissu watakuwepo.
Najua tuna tofautiana kwenye hili karibu hoja zake zote hazikuwa na mashiko. Zilikuwa populist ili kuwavutia wenye grievances zao. Na nyingine hazifanyi kazi context ya kwetu.
Siasa za upinzani ni ngumu na zinahitaji mtu ruthless kama Mbowe. Hauwezi kuwachekea watu kama Msigwa halafu ukategemea mafanikio. Au watu kama Sumaye. Usahihi wa hatua zake umethibitishwa na wao kuhamia CCM. Ila lazima kuna watu innocent ambao wameumizwa. Kwenye hilo inabidi awaombe msamaha.
Amandla...
Ila Mbowe ni kama kadata. Sasa hizo ndio sera?Alimuhonga Ujumbe wa kamati Kuu 🐼
Kulihitajika sana kuweko mtu ambae ana organise na ku manage mambo. Mbowe anajijua kuwa hana charisma ya Lissu. Mtu wa kulaumiwa hapa ni Lissu ambae alitakiwa aongoze mapambano on the ground. Badala yake akawa zaidi Belgium, New York na mtandaoni. Sasa ndio tunajua alikuwa amesusa na kumuachia Mbowe iki aweze kumruka kimanga...kufanya mambo nyuma ya pazia ndiko kulikosababisha kusiwepo na connection kati ya umma na maridhiano.
..maridhiano yalikosa shinikizo, na msisitizo toka kwa umma, na hali hiyo ndiyo inayowapa kiburi CCM.
..Pipoz Pawa ilikosekana wakati wa maridhiano. Pia imepotea tangu Mbowe atoke gerezani. Mazingira hayo ndiyo yamepelekea watu kuamini katika mtu mwenye haiba na misimamo kama ya Tundu Lissu.
Kulihitajika sana kuweko mtu ambae ana organise na ku manage mambo. Mbowe anajijua kuwa hana charisma ya Lissu. Mtu wa kulaumiwa hapa ni Lissu ambae alitakiwa aongoze mapambano on the ground. Badala yake akawa zaidi Belgium, New York na mtandaoni. Sasa ndio tunajua alikuwa amesusa na kumuachia Mbowe iki aweze kumruka kimanga.
Tofauti na watu mnavyoamini, Lissu hajaonyesha huo ujasiri wa kupambana na serikali face to face kama alivyoonyesha Mbowe.
Kinacho nisikitisha mimi ni kuwa team ya Mbowe na Lissu ingeweza kuitingisha CCM. Hizi misguided efforts za kumtoa Mbowe kwa nguvu zimerudisha nyuma sana hizo juhudi.
Amandla...
Rais,Wakuu wa Mikoa,Mawaziri,Mabalozi,Wakuu wa taasisi zote za umma.....Kila Kitu ndio nini Bwashee 😂
Ndio wako huko au Wewe huwaoni? 😂Rais,Wakuu wa Mikoa,Mawaziri,Mabalozi,Wakuu wa taasisi zote za umma.....
Hivi kati ya Heche na Wenje nani anatakiwa kuonywa!?Kwa nini ukimbilie ni hongo usione alimuona atafika mbali yanii Maono...anamtaka kijana awe nidhamu huku vile vile ajijenge kisiasa ndani ya chama
Majaliwa ni Profesor au Mama ?.Ndio wako huko au Wewe huwaoni? 😂
Shida yangu ni nani aliwazuia kuingia mtaani baada ya Mbowe kukiri kuwa hamna faida ya kuendelea na mazungumzo? Huo si ndio ingekuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kuonyesha nguvu za pipoz pawa?..Mbowe na wenzake walitofautiana jinsi ya approach ya maridhiano.
..kuna upande uliokuwa unataka maridhiano ya nyuma ya pazia vs upande unaotaka maridhiano yenye msukumo wa pipoz pawa.
..baada ya tofauti hizo ndio kukaanza minyukano, na kushughulikiana, kupitia chaguzi za chama.
..mwanzo minyukano ilikuwa ya siri, sasa imefika hatua ambako haiwezi kufanyika mafichoni tena.
Shida yangu ni nani aliwazuia kuingia mtaani baada ya Mbowe kukiri kuwa hamna faida ya kuendelea na mazungumzo? Huo si ndio ingekuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kuonyesha nguvu za pipoz pawa?
Amandla...