Mbowe: Niliona John Heche anapotea kisiasa, nikamteua Mjumbe wa Kamati Kuu

Basi ndio sababu alitaka kumfanya Heche awe chawa wake 🐼
Heche ni mhuni,hivi unajua alidanganya wanachama eti wanalamba 3 milioni per kikao kumbe walikuwa wanapokea 250,000 tu.

Baada ya kubanwa kwanini anasema uongo akasema eti alikuwa anatania.
 
Heche ni mhuni,hivi unajua alidanganya wanachama eti wanalamba 3 milioni per kikao kumbe walikuwa wanapokea 250,000 tu.

Baada ya kubanwa kwanini anasema uongo akasema eti alikuwa anatania.
Anamzidi Mbowe kielimu πŸ˜‚
 
FAM anashinda tena
 
Mbowe kila siku ni mtu wa nyuma ya pazia. Wakina Lissu na Lema walidanganyika na Club House. Kule wamejaa watu wa nadharia na sio watekelezaji. Na unfortunately hawaruhusu dissent.

Akifanya hivyo itaonekana kama ka capitulate. Akishinda watajadili kwenye vikao maana watu wa Lissu watakuwepo.

Najua tuna tofautiana kwenye hili karibu hoja zake zote hazikuwa na mashiko. Zilikuwa populist ili kuwavutia wenye grievances zao. Na nyingine hazifanyi kazi context ya kwetu.

Siasa za upinzani ni ngumu na zinahitaji mtu ruthless kama Mbowe. Hauwezi kuwachekea watu kama Msigwa halafu ukategemea mafanikio. Au watu kama Sumaye. Usahihi wa hatua zake umethibitishwa na wao kuhamia CCM. Ila lazima kuna watu innocent ambao wameumizwa. Kwenye hilo inabidi awaombe msamaha.

Amandla...
 
Halafu kitu kibaya zaidi wafuasi wake wanasema Heche kaongea vizuri sana kwa kumuheshimisha yeye MWAMBA, lakini MWAMBA Mwenyewe anasema HECHE anamtukana.
Amesema wapi kuwa Heche amemtukana? Mbona mnaleta uongo wa kijinga? Mbowe amesema kuwa Heche alisema uongo kuwa wanalipwa mamilioni wanapohudhuria vikao vya maridhiano. Alipobanwa, akasema alikuwa anatania. Na haya yalitokea kabla ya haya mambo ya sasa.
Kwa nini mnakuwa waongo waongo?

Amandla...
 

..kufanya mambo nyuma ya pazia ndiko kulikosababisha kusiwepo na connection kati ya umma na maridhiano.

..maridhiano yalikosa shinikizo, na msisitizo toka kwa umma, na hali hiyo ndiyo inayowapa kiburi CCM.

..Pipoz Pawa ilikosekana wakati wa maridhiano. Pia imepotea tangu Mbowe atoke gerezani. Mazingira hayo ndiyo yamepelekea watu kuamini katika mtu mwenye haiba na misimamo kama ya Tundu Lissu.
 
Kulihitajika sana kuweko mtu ambae ana organise na ku manage mambo. Mbowe anajijua kuwa hana charisma ya Lissu. Mtu wa kulaumiwa hapa ni Lissu ambae alitakiwa aongoze mapambano on the ground. Badala yake akawa zaidi Belgium, New York na mtandaoni. Sasa ndio tunajua alikuwa amesusa na kumuachia Mbowe iki aweze kumruka kimanga.

Tofauti na watu mnavyoamini, Lissu hajaonyesha huo ujasiri wa kupambana na serikali face to face kama alivyoonyesha Mbowe.

Kinacho nisikitisha mimi ni kuwa team ya Mbowe na Lissu ingeweza kuitingisha CCM. Hizi misguided efforts za kumtoa Mbowe kwa nguvu zimerudisha nyuma sana hizo juhudi.

Amandla...
 

..Mbowe na wenzake walitofautiana jinsi ya approach ya maridhiano.

..kuna upande uliokuwa unataka maridhiano ya nyuma ya pazia vs upande unaotaka maridhiano yenye msukumo wa pipoz pawa.

..baada ya tofauti hizo ndio kukaanza minyukano, na kushughulikiana, kupitia chaguzi za chama.

..mwanzo minyukano ilikuwa ya siri, sasa imefika hatua ambako haiwezi kufanyika mafichoni tena.
 
Kwa nini ukimbilie ni hongo usione alimuona atafika mbali yanii Maono...anamtaka kijana awe nidhamu huku vile vile ajijenge kisiasa ndani ya chama
Hivi kati ya Heche na Wenje nani anatakiwa kuonywa!?

Hapa ndipo mwamba anapoteza heshima yake
 
Shida yangu ni nani aliwazuia kuingia mtaani baada ya Mbowe kukiri kuwa hamna faida ya kuendelea na mazungumzo? Huo si ndio ingekuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kuonyesha nguvu za pipoz pawa?

Amandla...
 
Shida yangu ni nani aliwazuia kuingia mtaani baada ya Mbowe kukiri kuwa hamna faida ya kuendelea na mazungumzo? Huo si ndio ingekuwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kuonyesha nguvu za pipoz pawa?

Amandla...

..minyukano ilianza baina yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…