Mbowe: Nimepata chanjo ya AstraZeneca, Serikali iharakishe kuchukua hatua za kuikabili COVID19

Mbowe: Nimepata chanjo ya AstraZeneca, Serikali iharakishe kuchukua hatua za kuikabili COVID19

Au hii chanjo ndiyo ilipelekea akaumwa sana mpaka kupotea kwa kipindi fulani, usikute damu ya mwenyekiti wetu iliganda.
Kuumwa ni sehemu ya mapito ya binadamu, hata wewe unaweza kuumwa na kupotea muda wowote. Rejea alipo Mwenyekiti wenu aliyekuwa na ulinzi wa vifaru na helkopta. Punguza maneno ya nyodo!!
 
Moja ya waTz wakwanza kujitokeza kuipata hiyo chanjo kwa hiyari wakati ikiidhinishwa nchini niko hapa. Silishwi propaganda za kijinga za siasa mimi. Afya yangu ni ya thamani sana. Sikubali siasa za kijinga ziitawale akili yangu hata siku moja.
 
Ameshapewa shea yake ya pesa huko nje sasa kaja kuishikia bango hiyo chanjo...
Chanjo alizo dungwa Mbowe zina walakini sana kwa kuwa hazikuwahi kufanyiwa majaribio ya muda mrefu,zinakimbizwa sokoni kwa lengo la kupiga hela ndefu sio kujali watu - ni suala ka muda tu wale wote walio jingiza kichwa kichwa wakadungwa chanjo za zinazo tengenezwa kwa kutumia teknolojia ya kijinetik

Tofauti na zile chanjo zinazo tengenezwa Urusi na Uchina ambazo zinatengenezwa kutumia proven conventional technique inayo tumika katengeneza chanjo miaka nenda rudi bila ya kuleta madhala kwa watumiaji-unlike mRNA based vaccines whose short and longterm after effects are highky unpredictable, Mbowe should be aware of the risks involved in being innoculated using AstraZenecca vaccines.
 
Huyu nae kaanza kuyumba namuonaga kichwa lkn kwa hiyo chanjo ha ha ha!
Kafanya vyema kudungwa. Itakuwa reference nzuri kwetu na bila shaka kupitia yeye itathibitika kumbe AstraZeneca haina shida kwa waTZ🙂
 
Kwa taifa masikini kama letu inambidi rais ajitahidi aagize wizara husika kuharakisha upatikanaji wa chanjo.

Corona ipo na siyo ya kufanyia mbwembwe wala kutafutia umaarufu

ukweli ni kwamba corona sio tatizo kubwa tanzania kama mnavolikuza and ofcourse nmeshaona watu waliokufa kwa corona kipindi cha magu ingawa wengine walizushiwa tu but ukweli ndo huo corona sio burden kwa tanzania na huenda watu wameshajenga herd immunity which is the best
 
Well done my Life chairman ,long live the great conqueror of the CHADEMA Empire,your voice is the voice of all wild beast, well done
 
Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema amepata chanjo ya #COVID19 ya Astrazeneca alipokuwa nje ya nchi kibiashara

Aidha amemshauri Rais Samia Suluhu Hassan aharakishe mchakato wa Uchunguzi dhidi ya Corona ili hatua stahii zichukuliwe mapema na kuepusha vifo vinavyoweza kutokea

Amesema awali wao walitaka nchi ichukue hatua stahiki sio kwa maana ya kuifungia nchi bali kuwa na vituo vya kupima watu, kuwa na ventilators za kutosha na vifaa kwa wahudumu wa afya ili kukabiliana na ugonjwa
Na bado Kuna ma mbumbumbu yata shabikia huu uongo et wao hawakutaka lockdown!kweli wa Tz tunaonekanaga mazoba sana na wanasiasa uchwara, hv siyo huyo na Genge lake walitika bungeni wakishindikiza lockdown?hv kweli tungekifungiwa tungekuwa wapi kipindi hiki ambapo dunia yote imeamua kufungua raia wake waendelee na maisha yao Kama kawaida?
 
Pamoja na woga wangu juu ya COVID 19 na athari zake lakini bado nafsi inajawa hofu na hizi chanjo.....nikiutazama utaratibu wa research za chanjo hadi uizinishwaji wake na namna hili jambo linavyopelekwa msobe msobe na wanasiasa.......ngoja tuone...
 
HILO LA Chanjo sisi hatutaki kabisa...Astra Zeneca huko Inaua watu mpaka wao wamesitisha isitumike..Tunashukuru umechanjwa nadhani umewakilisha inatosha.

HILI LA Corona Kwa Hapa Kwetu twende Na approach ya kwetu sio kukimbilia huko.Na Mjue Hata Kenya wamekopa sana huko IMF na Bank ya Dunia.Mkimshinikiza Mama Kuhusu Machanjo akienda kukopa msilaumu mana Budget ya CHANJO HATUNAAAÀ...

MICHANJO HATUTAKI SISI..
 
Hotuba ya Mbowe mengi kasema ya msingi sana.

Yanatakiwa kutekelezwa.

Lakini pamoja na uzuri wa hotuba.

Kachomekea udalali wa chanjo ya Corona AstraZeneca.

Tena kaipamba kwamba hata yeye kachoma hiyo kwahiyo anatushawishi tuikubali hiyo! Huu ni udalali wa waziwazi.

Kulikuwa na haja gani kuitaja aina ya chanjo? Katika free market yeye ni nani kwenye Zeneca?

Mataifa mangapi wameikataa Zeneca kwa ubovu, iweje yeye ainadi kwetu?

Inchi ngapi wamesitisha hiyo chanjo ya Zeneca, kwanini yeye aipigie upatu?

Siamini kama mbowe alitamka hayo kwa bahati mbaya Bali alikusudia kuipigia chapuo.

Yamkini hata hakuchoma Zeneca lakini kwa vile kampuni ya Zeneca inatafta wateja huenda mbowe kakubali kuwa dalali kwa faida zake.

Zipo chanjo nzuri nyingi tu lakini siyo Zeneca!

Kuna Mordena, Pfizer etc!

Zeneca ya Mbowe ni uchafu hautakiwi hata kuwekwa kwenye mapendekezo.

Udalali wa mbowe Takukuru Chunguzeni tutapigwa na mchaga huyu.

Hana tofauti na yule Meku anaedalalia majeneza pale mhimbili!
 
Back
Top Bottom