Mbowe: Nimetoka Gerezani kwa moyo mweupe. Katiba ni ajenda yetu, Sisi sio magaidi

Upendo alimshinda Constantine mbali sana. Ila maelekezo ya mtaka yote kwa pupa yaliharibu sana

Kweli kabisa mkuu. Hili nililiona nikajiuliuza Kama Geita mgombea wa Chadema anapata kura zote hizi je maeneo mengine?. NEC walifanya kosa kubwa Sana.
 
Mtamtukana mbowe lkn kwa uzoefu wangu mbowe Ni mmoja was magwiji wa siasa za tz. Level zake Ni akina hayati maalim, mwl nyerere , Mzee malecela na wachache Sana. Lisu siasa zake Hana tofauti na Dk. Slaa. Amuige Mr mbowe.
 
Chunga ulimi wako, una maana Rais katoa rushwa? bakshishi? Mbona mnakosa nidhamu?
 
Hakika chadema ni mpango wa Mungu kuwaokoa watanzania dhidi ya majambazi meusi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa hiyo hicho ndicho kamati kuu iliongea ? Kuanzia mwanzo hadi mwisho waliongelea mambo ya Mbowe?
 
Chama kitakachoishinda CCM au kukitoa madarakani.

Ni ngumu sana,,labda vyama vyote viungane kwa pamoja, na wagombea wake watokee pwani, kanda ya magharibi na kanda ya ziwa hapo atleast. Lakinii kwa chadema tu co rahisi, kwani ninavyoona wafuasi wake wengi hutokea kaskazini tu,, Tanga sidhani kama kuna wafuasi wengi, labda wa kuokota okota.

Binafsi, mara elfu kumi ccm iendelee kutawala kuliko chadema, na mama yetu aliongoze taifa letu hata kwa miaka 30 mbele sawa tuu,, tunampenda sana, ni mtu wa watu.
 
Siku ya kwanza kumuona Mbowe ilikuwa ni Jangwani Dar es salaam kwenye mkutano wa wabunge wa vyama vya upinzani,siku hiyo alijiita sauti ya zege.Walukuwepo akina Danyakanga,Mutungirehi,Aman Warid Kaburou nk.Kuanzia pale niliona Kuna kiongozi na mzalendo ndani ya Mbowe.Hadi Leo ,mtazamo huo haujabadirika.Kweli Mbowe ni kiongozi na mzalendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…