Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Kwa hilo la Covid 19 mheshimiwa Mbowe angekubali tu matokeo kwamba kazidiwa.Upamoja wa wananchi na raisi Magufuli katika hili ni ushahidi tosha kwamba Raia wapo pamoja na raisi wao.


Maadamu yeye mheshimiwa Mbowe alishalizungumza basi na aliache na hata km madhara yatakuwepo huko mbele atakuwa shujaa kwa sababu historia itamlinda.


Kwa yeye kuendelea kulisemea mara kwa mara italeta picha km analibeba hilo kama agenda ya kisiasa.
Tatizo sio RAIA kuwa na nani Bali ni kuwa wako sahihi na wanakoelekezwa? Rais anasema ugonjwa unaisha, lakini madereva wetu kwa idadi kubwa wakifika mipakani wanagundulika wagonjwa kwa nini?
Na hao wote wanatoka kwenye jamii huku mitaani ambako hatupimwi!
US embassy wameonya RAIA wao kuwa hali ya Dar inatisha, nchi jirani wanafunga mipaka bado hatuamini, lakini tunamuamini Magufuli tokea huko mafichoni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe mbona hatupi takwimu za Corona za ukoo wake wa Mbowe za idadi ya waliopimwa,waliougua,waliopona, waliofariki na rate ya maambukizi imepungua au imeongezeka kwa kiasi gani ? Hizo hazihitaji serikali ni yeye tu kuzitoa
Tunaziomba ili tuone jinsi hili janga lilivyo kubwa kwenye ukoo wake

Ukoo wake unaficha? mbona hatupi hizo takwimu hata siku moja tunaomba awe anatupa takwimu za kila siku
 
Trend imetokea wapi?? Usiulize..trend ipi wakati VIPIMIO VYA VIPIMO VINAPIMWA??

Nilichogundua ukiwa Mr Politishiani, unakuwa pathological liar...

Everyday is Saturday........................ 😎
Ajabu tukipimwa mipakani maambuzi tele kwa madereva wetu sasa badala ya kupima mapapai na mbuzi na mafenesi kwa nini tusiangalie usalama wa madereva wetu na kuwapima tuna viongozi sio kabisa
 


Akizungumza na taifa Leo hii, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema na kiongozi wa upinzani bungeni Mheshimiwa Freeman Mbowe amemfafanua vizuri Spika wa Bunge kuwa ni MTU wa aina gani.
Akizungumza kwa upole mkubwa, unyenyekevu na weledi wa hali ya juu ameeleza vituko na udhalilishaji ufanywao na Ndugai kama vile gubu la ukewenza.
Hakika Mbowe utulivu usio na chuki umewashangaza wengi kwani utadhani hakuna jambo baya hata moja kesha wahi kutendewa yeye na chama chake.
Tupende tukatae, Mbowe ni kiongozi. Tena kiongozi adimu kupata kutokea katika zama hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbowe analialia sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hana lolote kasikia mabeberu wanaongelea kufungua na yeye anataka kufungua wakati hata mashine mbovu inayopima mapapai positive hajaibadirisha intubators hana na hata mpango mkakati w kitaifa wa kupambana na janga hana
wewe mkorofi kwani ni nani asiekujua.
lawama zoote unampa rais wakati yeye ajaleta corona.kaka kwani vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimejaribu kujizuia nimeshindwa.

Tanzania inaenda kuangamia kwa kukosa maarifa.

nilikuwa nasubiri nipewe ripoti ya mashine za kupimia ambapo kila takwimu zilizokuwa zinatoka ugonjwa ulikuwa unaongezeka maradufu.

tujiulize km wagonjwa wamepungua je tulipima wangapi na kwa mashine zipi?

Tunaomba viongozi watuambie sisi wananchi je ripoti ya ukaguzi ya mashine imetoka?

na wakaanza kupima tena lini?

najiuliza sipati majib pale mashabiki watakapojazana viwanjani, wanafunzi maskulini na wageni kuingia bila karantini hii ni jambo la kustia mno.


salaam.
0F7204B4-12D3-418E-9ADF-1D7EE8DAF1F2.jpeg
 
Hivi unafikiri Ripoti hiyo utaisoma muda huo huo Rais anapoisoma? Rais anapata taarifa mapema sana hivyo kuhoji Ripoti imetoka au laah ni kukosa maarifa kwenyewe.

Je, uliambiwa upimaji usingefanyika kipindi wanafanya huo uchunguzi?
Ndicho ttulichooambiwa!
 
huyo mbowe ni punguani tu, anasema watu wanakufa mbona mwanae kapona au yeye alitibiwa america
 
Kwani suala hili halikugusi ndugu kwa haya yanayoendelea.

Uliwahi kumuona waizir mkuu wa italia akilia hadharani huu ugpnjwa ni hatari siasa haipaswi kuwekwa mbele bali fact,truth na Science
Ni hatari kweli ila kwa aliyoyasema Rais wetu leo, basi huu ugonjwa unaelekea kudhibitiwa hivyo ondoa hofu.
 
Mimi sio CCM lakini kwa maono yangu huyu Mbowe naona kama anawapoteza watu jamani.
Yaani Kiongozi mkuu wa Nchi, Rais aliyeaminiwa na kupewa mamalaka na wananchi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania anazungumza tena kwa kutumia fact bila kupepesa macho akijaribu kuelezea hali halisi ilivyo katika kujaribu kuwatuliza wananchi na kuleta matumaini.

Mbowe anajitokeza kudai kwamba nchi inaenda kuangamia kwa sababu ya Corona huku kiking'ang'ania Lockdown kwa sababu chenyewe kina uhakika wa kula na kwenda chooni.
Kwani hujatosheka ulivyokaa karantini?

Nchi hii ina wanasiasa Uchwara wenye njaa tu ya madaraka wanaopigia debe matumbo yao kwa kivuli cha kujifanya wanapigania haki za wananchi, hao wananchi unaowapigania hujui maisha yao? unavyong'ang'ania Lockdown lengo lako ni nn? Tufe na njaa ama?... Kuna wanasiasa visambugile kweli 😁.
 
Hivi tutakapo kufa kwa hayo maelfu wewe utafaidi nini?? Autuseme weye hutakufa? Zidi kuombea wenzio vifo ila na weye utakufa tu. Kumbuka hata kama upo nchi za nje, hakuna mahali corona haijafika hivyo usijione salama sana huko. Tunataka kusikia habari njema tena hizi za kufa kufa tu zimetuchosha.
Kuna watu utafikiri wanakula maiti!
 
Kwani suala hili halikugusi ndugu kwa haya yanayoendelea.

Uliwahi kumuona waizir mkuu wa italia akilia hadharani huu ugpnjwa ni hatari siasa haipaswi kuwekwa mbele bali fact,truth na Science
Waziri mkuu wa italia hajawahi kulia hadharani. Ile ni fake news tu. Yaan taifa la watu milioni 60 na ushee, wafe watu 40000 halafu waziri mkuu alie hadharani, hiyo inakuingia akilinj kweli?

Tena kipindi hicho wanatoa uzushi huo wagonjwa walikuwa hawajafika hata laki moja italia.
 
Hao ni wazee wa kumlaumu,

Siku Mbowe anavaa gloves sijui alisomea wapi udaktari
 
ugonjwa unakuzwa sana kwa kuwa unawala sana super power US,europe,,africa sio saana kivilehapo kariakoo mbona hawaanguki na kufa kama kuku wa mdondo ?ni mwezi wa tatu sasa kariakoo kuna nyomi mwanzo mwisho.manzese.tandika sokoni.manzese njia ya kwenda majoe ni nyomi,

acha kufata propaganda za mitandaoni.africa ni nchi chache sana zenye vipimo vya uhakika.vipimo vingi ni batili.africa ukikutwa na corona ukitibiwa ukapona unaachwa kuja uraini kuambikizwa tena,kazi gani sasa hii,
wameshindwa super power US na europe wataweza zambia.
lakini pia lazima maisha yarejee iwe corona ipo au haipo ndege zitaruka na viwanda vitafanya kazi na watu watasafiri ila kwa kufata utaratibu maalum.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwa hiyo unadhani Magu anaficha data za vifo vya mapapai na mafenesi si ndiyo mkuu?
 
Back
Top Bottom