Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Mbowe: Rais, wanaopinga ushiriki wa Taifa kwenye vita ya Corona wanawaza uchaguzi na huruma yako ktk uteuzi. Ukweli lawama zote zitakuangukia wewe

Hivi unafikiri Ripoti hiyo utaisoma muda huo huo Rais anapoisoma? Rais anapata taarifa mapema sana hivyo kuhoji Ripoti imetoka au laah ni kukosa maarifa kwenyewe.

Je, uliambiwa upimaji usingefanyika kipindi wanafanya huo uchunguzi?
Walitumia vipimo vipi wakati hivyo vilivyokuwepo ni fake ?

Au walikuwa wanapima kwa kupiga ramli ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hajavaa barakoa anavaa gloves nyeusi
==============
Atueleze hiyo njia inapambana na covid19 kiaje sababu huko kwa wenzetu mabingwa wa kufanya hivyo hali si hali.
 
Kutoa takwimu? Ni silaha? Binafsi sioni kama hiyo ni silaha, tena iwe ya kwanza. Pengine watu kuwa aware juu ya huu ugonjwa kulitakiwa kupewa kipaumbele kuliko takwimu.

Watu kuwa aware kulitakiwa kuwe ni ubwabwa na maharage halafu takwimu ziwe ni kachumbari ya huo ubwabwa na maharage.
 
Unanikumbusha story moja mbuni alikuwa anafukuzwa na simba akaona option ya kusurvve ni kufikia kichwa chini ya mchanga akiamini amejificha kumbe body yote ipo exposed unajua nini kilitokea?
Simba akampita......
 
hawaruhusu kama unavyofikiria wewe kuna utaratibu maalum utakao zingatiwa wa kitaalam utakaofatwa.
corona haishi leo wala kesho ni lazima maisha yaendelee huku kukiwa na tahadhari kubwa.

magufuli anaanzisha ila hamini nakwambia kuna nchi nyingi tu zita fuata,


Sent using Jamii Forums mobile app
Amini akuna utaratibu wala ushauri wa wataalam, kwa kuwa tumeamua kumshangilia nae ndio anatekeleza tu, tuendelee tu kumshangilia atakapo tufikisha tusiulizane!
 
Mheshimiwa ameshaongea Jana kwamba Tume ya kuchunguza iliundwa na waziri wa afya na majibu wameyapata kwahiyo atatangaza yeye Mwenyew waziri Mwenye dhamana.
Ila natabiri majibu yatakuja kwamba tatizo ilikuwa wataalamu hasa Yule aliyetumbuliwa ili kujustify takwimu zilizopo na zilizosemwa Jana na mheshimiwa Rais kwamba Ni sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WHO walitabiri hali yetu waafrika kuwa mbaya, Bill gates na Melinda gates wakatabiri tutakufa na kuzagaa mitaani.
Mungu ni mwema utabiri wao haujatimia, sikushangai mchawi kama wewe unayeiombea nchi mabaya utabiri wako Mungu atautupilia mbali kuleee.

Kuna mitanzania ya hovyo sana kutwa kutamani mabaya yatokee utadhani haina ndugu wala familia, unadhani yakitokea mabaya unamkomoa adui yako wa kisiasa pekee?


Sent using Jamii Forums mobile app
hupendi taarifa mbaya ila hali ndvyo inavyoeda kuwa
 
hawaruhusu kama unavyofikiria wewe kuna utaratibu maalum utakao zingatiwa wa kitaalam utakaofatwa.
corona haishi leo wala kesho ni lazima maisha yaendelee huku kukiwa na tahadhari kubwa.

magufuli anaanzisha ila hamini nakwambia kuna nchi nyingi tu zita fuata,


Sent using Jamii Forums mobile app
Hamini[emoji808]
Amini[emoji818]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amini akuna utaratibu wala ushauri wa wataalam, kwa kuwa tumeamua kumshangilia nae ndio anatekeleza tu, tuendelee tu kumshangilia atakapo tufikisha tusiulizane!
itakavyokuwa ndo hivyo hivyo mtakao kufa mfe na tutakao pona tupone lakini maisha lazima yaendelee.
hii ni vita tumevamiwa na adui corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 

HOTUBA YA MBUNGE FREEMAN MBOWE KWA UFUPI

Nimezungumza na Rais kwenye simu nimemuambia tafadhali shirikisha Jamii pana ya Watanzania ili jambo tulibebe wote, huu ni msiba na msiba haachiwi Mtu mmoja, kwa nia njema kabisa, tushirikiane kwa pamoja kwenye mapambano haya dhidi ya virusi vya corona.

Mhe. Rais unafiki haujawahi kuliacha taifa lolote salama, usikae wakati wote ukafikiri sisi ambao tunajaribu kukushauri, kuikosoa Serikali yako na kuilekeza, eti tuna nia mbaya au nongwa na wewe, hapana! , tunafanya hivi kwa nia njema na mapenzi sana kwa nchi yetu."

Mhe. Rais lawama zote za janga la Corona zitakuangukia wewe, huu ni ukweli wa Mungu na mimi kama Mbowe, mtu mdogo sana katika nchi yetu, nikwambie Rais wangu, wanaopinga ushirika wa taifa katika vita hii wanawaza uchaguzi na kuomba huruma yako katika uteuzi.

Nasikitika kwa niaba ya CHADEMA kwa namna ushauri wetu wa kuwataka Wabunge wajiweke karantini ulivyopokelewa vibaya na kuonekana tunashindana, Spika ametumia majukwaa mbalimbali kunishambulia na kuninidhalilisha mimina Viongozi wenzangu bila kuiona nia yetu njema.

Spika kila akitaka kuahirisha Bunge lazima apande na Mbowe, tumekutana Bungeni na Spika miaka 20 iliyopita sijawahi kumvunjia heshima hadharani wala sirini, nimesoma Kibaha na Spika amesoma pale ni mwanafunzi mwenzangu wa shule moja, namuheshimu,naliomba Taifa kumuombea.

Tuligoma lockdown tukashindwa hata kufanya partial lockdown na tukaruhusu ugonjwa kuenea na kuua wapendwa wetu, tulidhani tunalinda uchumi wetu na kusahau uhai wa watu wetu, sasa Corona inaendelea kutula wote, inakula uchumi wetu tupende tusipende.

Namshukuru Mungu kwa sasa Mwanangu ambaye alikuwa mgonjwa wa corona hatimaye amepona baada ya kukaa karantini kwa siku 57 nina uhakika amejifunza mengi, Familia nayo imejifunza mengi, nawashukuru Madaktari na wahudumu wengine

Kufuatia kikao hiki, Kamati Kuu imejadili kwa kina, miongoni mwa agenda mbalimbali, Janga la Corona na athari zake kwa taifa letu, mataifa ya jirani na dunia nzima katika ujumla wake.

Kamati Kuu,ilijiridhisha kuwa janga hili halihitaji masihara, mzaha wala usiri katika kulikabili.Ilitambua kwa mara nyingine umuhimu wa kuweka tofaui zetu pembeni na kutoruhusu chuki za kisiasa, hodhi za kisiasa, kiburi cha madaraka na mamlaka katika kupambana na vita hii.

Mwisho
kumbe leo amejua unafiki na uzandiki si mzur katika taifa.
 
Back
Top Bottom