Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kinachoendelea katika ajira ya Watumishi ni kukatwa kodi mara mbili.

Hizi hapa nukuu za Mbowe...

“Tunapowapa Watawala nafasi ya kuongoza maisha yetu na wanaamua bila kujali kinachotupata, hatupaswi kuwa waoga.

Kuna wakati nakwazika sana kwa kazi ninayofanya mnapokuwa waoga na hofu, halafu mnalalamika.

Hao wanaowatoza kodi hiyo wanakwenda kununua V8 ya Shilingi Milioni 450 au 500, mtu ambaye angekuwa nyumbani kwa mumewe au mkewe asingeweza kununua V8.

Lakini kwa kuwa kuna pesa ya Wajinga Watanzania wanaweza kununua gari la kumpa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi, Jaji kila mmoja.

Jiulizeni ni Wafanyabiashara wangapi ambao wana uwezo wa kuendesha magari mapya?

Magari mapya Nchi hii ni mali ya viongozi wa Serikali, na mnavyokaa kimya mambo haya ndiyo yanaendelea, mnatakiwa kuamka.

Kama mnataka kuibadilisa Nchi hii lazima tuache woga, lazima viongozi wa dini muongee.

Nilimwambia Rais Samia hii simulizi ya ‘amani’ ‘amani’ ‘amani’ ni kupoteza muda, simulizi sahihi ni haki haki haki.

Kuwepo na haki kwa watu wote litakuwa tafa bora la kuishi. Watanzania wameangalia uchaguzi wa Kenya kila mmoja ametamani, ulikuwa wa wazi hakuna mizengwe
 
Baadae atampigia mama simu amwambie asimuelewe vibaya, ameamua kujitokeza ili kuwazubaisha na kuwahadaa wadanganyika, baada ya malalamiko mengi juu ya ukimya wake.

Kalagha baho kwa wale wote wanaofikiri kuwa Mbowe alimaanisha. Siku Mungu akimchukua wengi mtashangaa mtaposikia wasifu wa cheo chake kweny kile kitengo cha "gizani".

Hata Mrema wengi walipinga juu ya utumishi wake pale kitengoni, tuliaminishwa kuwa ni kiongozi wa upinzani alienyima mzee Mwinyi usingizi mwaka 1994 to 1995.
Lkn juzi kila kitu kiliwekwa wazi baada ya kifo chake, alikuwa mtumishi alietukuka pale kitengoni. RIP Mrema umetuachia somo la kujitafakari upya kuhusu huu upinzani butu wa Tanzania.
 
Hii kauli ya Mbowe kwamba "nakwazika sana kuona wanakuwa waoga" inaonesha bado ana dhamira ya dhati kuleta mabadiliko nchi hii.

Kinachomkwamisha ni kukosekana kwa ushirikiano anaohitaji toka kwetu, tupo kama misukule kumbe naye anajua hilo japo ameshindwa kulitumia hilo neno kwa heshima yake aliyonayo kwetu.

Naamini wale wajuaji wanaosema kila siku Mbowe amelamba asali ndio maana yupo kimya, sasa ni wakati wao kum-prove wrong Mbowe, simameni mhesabiwe kulinda haki zenu ili Mbowe awe pamoja nanyi.
 
Hii kauli ya Mbowe kwamba "nakwazika sana kuona wanakuwa waoga" inaonesha bado ana dhamira ya dhati kuleta mabadiliko nchi hii.

Kinachomkwamisha ni kukosekana kwa ushirikiano anaohitaji toka kwetu, tupo kama misukule ndio maana naye anajua hilo, japo ameshindwa kutumia hilo neno kwa heshima yake aliyonayo kwetu.

Naamini wale wajuaji wanaosema kila siku Mbowe amelamba asali ndio maana yupo kimya, sasa ni wakati wao kum-prove wrong Mbowe, simameni mhesabiwe kulinda haki zenu ili Mbowe awe pamoja nanyi.
Bavicha ndio wanamkwamisha Mbowe, ni waoga kupitiliza
 
I dont believe in my fellow human again.

Nilianza na Dr. slaa, akasaliti kambi!

Siasa hasa z kiafrika sio za kuamini kwa 100%.

wakiwekewa dau mezani wanabadilika
Mbowe ameshazungumza kuonesha msimamo wake, ajabu nyie bado mnaamini hisia zenu, hebu acheni kuishi kama mnatembea barabarani huku mnaota ndoto mchana wa jua kali, amkeni!.
 
Kuwatetea watanzania na utegemee wakuunge mkono ni sawa na kusubiri embe chini ya Mwarobaini au kupiga mbizi kwenye lami.
Watanzania ni wanafiki wa kutupwa
Namshauri Mbowe aendelee na Biashara zake na aipe muda familia yake kufurahia naye maisha,ametumia muda mwingi kutetea wanafiki.
CCM itaondoka siku JWTZ wakielewa wajibu wao wa kulinda katiba kwa kuelewa yaliyoandikwa ndani na siyo kusoma cover la nje tu
 
JWTZ,POLISI ,WALIMU wanachelewesha maendeleo
 
Ni kweli kuwa wananchi ni waoga ila siamini kama Chadema inaweza fanya jambo lolote la maana katika Taifa letu kwa sasa.

Chadema imeshindwa kufanya lolote ilipokuwa ya moto kwa sasa viongozi wake wakuu wamejichokea na kukata tamaa.
 
Anacheza pande zote mbili, huku asiharibu na kule pia asiharibu, yupo vuguvugu, lkn mwisho wa siku Mbowe ni sehemu ya Utawala uliopo, ni sehemu ya Tozo na yuko kwa ajili ya kuwachanganya na kuwatumia Wachaga wenzake kama ngazi tu ili kulinda na kuhakikisha Utawala uliopo unafanikiwa, pure evil!
Ulitaka wewe ukae kimya halafu Mbowe aseme peke yake na akikamatwa humsaidii. Pathetic!!
 
Back
Top Bottom