Mbowe: Tozo ya benki, wafanyakazi wanakatwa kodi mara mbili, wanaotoza kodi wanaenda kununulia V8 ya milioni 450 au milioni 500

Wewe ndiye mwenye maono sahihi. Mbowe Hana jeshi .la kumsaidia zaidi ya support toka kwetu wananchi lkn tupo tu kama mazuzu. Mbowe wa watu anafika mahali anachoka
 
Kama ni hivyo angeweza pia kuamua kukaa kimya tu badala ya kuhadaa watu ambao tayari wana shida na wanaumia, siyo vizuri kumkejeli mtu ambaye anataabika tayari!
Mtu anayetaabika halafu halalamiki wala kudai haki yake inafaa akejeliwe ili akili imkae sawa. Kwasabb hawa hawa wananchi wanaoumia ndiyo uchaguzi ukifika unakuta akili zinafubazwa na ubwabwa, kanga na kofia
 
Mtu anayetaabika halafu halalamiki waka kudai haki yake inafaa akejeliwe ili akili imkae sawa. Kwasabb hawa hawa wananchi wanaoumia ndiyo uchaguzi ukifika unakuta akili zinafu azwa na ubwabwa, kanga na kofia

Hajaombwa lakini, angeweza kukaa kimya tu kama wenzake akina Zito, Tundu Lisu & Co. wakiendelea kula matunda ya kazi yao hamna haja ya kujifanya unajali matatizo ya watu wakati ni uongo, it’s just not right!
 
I dont believe in my fellow human again.

Nilianza na Dr. slaa, akasaliti kambi!

Siasa hasa z kiafrika sio za kuamini kwa 100%.

wakiwekewa dau mezani wanabadilika
Ndio maana kawaambia mnapaswa kuacha woga nyie mnaokatwa matozo,sasa unayeumia wewe halafu unataka usubiri kumuamini mtu adai haki zako.
 
Ni kweli kuwa wananchi ni waoga ila siamini kama Chadema inaweza fanya jambo lolote la maana katika Taifa letu kwa sasa.

Chadema imeshindwa kufanya lolote ilipokuwa ya moto kwa sasa viongozi wake wakuu wamejichokea na kukata tamaa.
Fanya wewe,achana na Chadema,unaitegemea Chadema ifanye jambo wakati wewe umejifungia chumbani kwako
 
Anatumia Kodi ya zetu? Kama ni hela ya biashara yake hakuna shida
Mbowe alikuwa waziri mkuu KIVULI, Kambi ya upinzani, Kodi zetu zilitumika kumnunulia Kwa mkopo magari hayo hayo.

Mbona hakuyakataa Yeye na Kambi yote ya upinzani??

Anapata wapi uhalali kuhoji magari ya kifahari???

Tunapoandika KATIBA mpya ya wananchi, yapo mambo hata viongozi tunaowashabikia lazima wadhibitiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…