Pre GE2025 Mbowe: Tunaweza kufanya maandamano ya shari endapo hatutosikilizwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Katika maandamano yaliyofanyika Mwanza, Februari 16, 2024, Freeman Mbiwe amesema "Tuna uwezo wa kufanya maandamano ya amani, lakini vilevile tuna uwezo wa kufanya maandamano ya shari. Nawaambia polisi na usalama wa taifa, waelezeni mabosi zenu, sisi kitu tunachokisema viongozi wa CHADEMA tunawasilisha hisia za mamilioni ya watu hawa."
Hii ni chadema huku hakuña machawa bei
 
Yaan kupanga maandamano halafu kuyafanya ni mafanikio ya kwanza!!!
Basi kama ndivyo, tatizo ni kubwa. Sidhani kama tunafanya maandamano ili kujifurahisha.
 
Katika maandamano yaliyofanyika Mwanza, Februari 16, 2024, Freeman Mbiwe amesema "Tuna uwezo wa kufanya maandamano ya amani, lakini vilevile tuna uwezo wa kufanya maandamano ya shari. Nawaambia polisi na usalama wa taifa, waelezeni mabosi zenu, sisi kitu tunachokisema viongozi wa CHADEMA tunawasilisha hisia za mamilioni ya watu hawa."
Muwe mnaweka na kauli za kiboya za yule boya lenu linalozunguka huko mikoani
 
Mwanasiasa sio mtu wa Mchezo mchezo

alipewa kandarasi ya miaka 7 kuutangazia Umma kuwa Mmasai ni Fisadi na akaifanya kwa ufanisi kuliko kazi yoyote nyingine

akapewa tena kandarasi ya Miaka 6 ya kumtangaza Ngosha kuwa ni Dikteta

akiwa kwny Public hujifanya anaempaga Kandarasi kuwa ni Adui yake

walipofurushwa na Ngosha walimtumia kuwasaidia kupata hifadhi nje ya Nchi na ngosha alipokatwa kichwa wakamtumia tena kuwasaidia kurudi

sasa hivi wanatumika tena kusaidia kupatikana kwa fedha za Millenium challenge

Lema alivyotaka kurudi eti alimpigia simu Jk
 
Katika maandamano yaliyofanyika Mwanza, Februari 16, 2024, Freeman Mbiwe amesema "Tuna uwezo wa kufanya maandamano ya amani, lakini vilevile tuna uwezo wa kufanya maandamano ya shari. Nawaambia polisi na usalama wa taifa, waelezeni mabosi zenu, sisi kitu tunachokisema viongozi wa CHADEMA tunawasilisha hisia za mamilioni ya watu hawa."
Wameona ya amani hayawapitii umaarufu kwenye media .ya vurugu watapata coverage ya BBC na voa
 
Wameona wananchi wametulia maandamano yamekosa mvuto sasa wanataka kuleta fujo wajaribu hayo maandamano ya shari ndio wataelewa .
 
Katika maandamano yaliyofanyika Mwanza, Februari 16, 2024, Freeman Mbiwe amesema "Tuna uwezo wa kufanya maandamano ya amani, lakini vilevile tuna uwezo wa kufanya maandamano ya shari. Nawaambia polisi na usalama wa taifa, waelezeni mabosi zenu, sisi kitu tunachokisema viongozi wa CHADEMA tunawasilisha hisia za mamilioni ya watu hawa."
Kwani Samia alichaguliwa na nani?
 
Jikite kwenye mada
Kwani kuna nini cha pekee hapo? Binadamu yeyote ana uwezo wa kuwa mstaarabu au kufanya vurugu. Ana uwezo wa kutumia mazungumzo au nguvu. Hilo ni jambo la kawaida sana.
 
Kwa hiyo Maandamano ya Amani hawajaridhika nayo, wanataka ya fujo.

Katika uhalisia, umafanya amani na ustaarabu kwa mtu anayethamini amani na ustaarabu. Kufanya ustaarabu dhidi ya mhuni, unakuwa unapoteza muda.

CHADEMA waendelee na maandamano ya amani huku wakipima kama CCM inaelewa lugha ya kistaarabu? Kama haielewi, basi lazima.kwenda kwa namna ambayo wataelewa.
 
Maandamano ya shari alikuwa anamaanisha nn?
Kwamba wataua watu njiani? Watapora watu njiani? Wataziba barabara?

Sidhani kama ilikuwa kauli sahihi kwa FAM
 
Back
Top Bottom