Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Pre GE2025 Mbowe: Uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA nilimpa gari yangu akafanyie kampeni. Nyumba ya Dodoma nilipewa na Serikali, nikampa yeye

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Amekaa jela muda gani wakati ameshinda kesi zake zote? Na nyingine amefutiwa. Sana sana amekaa mahabusu. Angalau Heche, Lema, na viongozi wa Bawacha na Bavicha wamepitia huko.
Amandla...
Nyumbu wa Sultan Mbowe mna bidii sana
 
Kugombea uenyekiti lissu anasimangwa saana, tumemchoka nkurunzinza tunataka changamoto mpya lissu atatusogeza mbele
 
Ni aibu sana Chama kinachotafuta dola kuongozwa na Disco Joker, tena mlevi, aliefeli form four? These people are not serious!.
Wakati ni ukuta, demokrasia ya ukweli ni kuachiana viti sio kulazimisha kuwa kiongozi, the big boss must go aache kulia lia, aje kijana alete changamoto mpya japo ana ulemavu!!

However, DJ akiweza kung'oka tafadhali mnitag!! Ni ngumu mno. Ni rahisi kijana kupita kwenye tundu la sindano kuliko kushinda hicho kiti cha m/kiti wa maisha wa ukoo. The boss can't let it go kirahisi itakuwa Vita kubwa na figisu kama zote nje na ndani ya uwanja!!
 
Mbowe kupitia Crown FM anasema kwenye uchaguzi wa kwanza Lissu akiwa CHADEMA Mbowe alimpa gari yake binafsi ili akafanyie kampeni. Pia anasema Nyumba aliyokuwa akiishi Lissu pale Dodoma ilikuwa yake aliyopewa na Serikali Ila akamuachia Lissu aishi yeye Mbowe akaenda kupanga.

View attachment 3194386
Ilikuwa na ni vyema sana viongozi wa kisiasa, kijamii, kifamilia kitaasisi hata KIROHO, kuwajenga na kuwaandaa watu wengine kwa uongozi. Hii tabia ya kung'ang'ania madaraka hata Nyerere hakuwa nayo. Ndiyo sababu ya migogoro duniani hasa Africa.
 
Yote haya ni Lissu kuchukua form ya kugombea uenyekiti,haya ngoja tusubiri Lissu naye afunguke yake hadi hiyo 21 January tutasikia mengi sana. Mbowe anajua kuchamba kama mzaramo vile.
Mbowe ana mengi dhidi ya Lissu na akiamua kufunguka, Lissu atarudi Ubeleji na kwenye uchaguzi hatakuwepo.
 
Kwa hiyo hizo ndio sababu za kugombea Uwenyekiti miaka zaidi ya 20.

Aisee shule ni muhimu. Mbowe kukosa shule kunampa tabu
 
Lissu nae alikubali kufa kwa ajili ya chama, lipo lubwa? Lissu ana risasi mwilini, hayo mbowe anaona ni kidogo?
Mtu mwenye risasi mwilini ndiyo anataka kuwa Mwenyekiti??? Yaani CHADEMA mumekosa watu wote ndiyo mnauletea mtu mwenye vyuma na shaba mwilini?
 
Mpaka sasa sijasikia sera yoyote kutoka kwa kambi ya Mbowe/Wenje zaidi ya kumuattack Lissu.

At least kutoka kambi ya Lissu/Heche nimesikia kuwa wanataka kutokomeza rushwa ndani ya chadema.Kutokomeza ufadhili wa chama cha mapinduzi kwa viongozi wa chadema.Kukirudisha chama kwenye misingi ya kuanzishwa kwake n.k

Halafu,ina maana Mbowe alikuwa anamfadhili Lissu ili awe chawa wake?Na sasa ana hasira nyingi na Lissu kwa kukataa kuwa chama wake?

Mpaka hapo tu unaona nani anafaa kuwa kiongozi wa chama hiki kwa sasa.
 
Sababu hizi zote hazina uhusiano kwa Lissu Kugombea Uenyekiti

Yaani Mbowe ulikuwa ukifanya hivyo ukiwa na hesabu za moja kichwani siyo?

Imekula kwako
Mkuu hizi sababu anazitoa kuonyesha ule msemo wa Kiswahili usemao "Mfafhili Mbuzi......"

Tuhuma za Lissu Mbowe hakuzitegemea..
 
Mbowe ana mengi dhidi ya Lissu na akiamua kufunguka, Lissu atarudi Ubeleji na kwenye uchaguzi hatakuwepo.
Mbowe huyu ambaye yuko mfukoni mwa Abdul au mwingi? Hii bishara ya mama Abdul na Sultan tunaifunga rasmi tarehe 21 January 2025
 
Kila mtu alishikwa mkono na mtu katika nyakati tofauti hakuna binadamu ambaye hajawahi kupata usaidizi.

Msaada sio kigezo cha kuzima fikra za mtu , Mbowe ajikite kupangua hoja kwa ustadi anachokifanya sasa hakina tofauti na wale vijana wake wawili waliomtia aibu juzi kwenye mdahalo wa Chief Odemba.

Namshauri Mbowe ajipange vizuri na yeye kwa mdahalo wa tarehe 18 , vinginevyo anaweza kutia aibu ya mwaka.

Lissu is not a walk in the park kwenye midahalo.
 
Mbowe Bwana, kwahiyo alifanya hivyo ili Lissu asigombee uchairman
 
Mkuu hizi sababu anazitoa kuonyesha ule msemo wa Kiswahili usemao "Mfafhili Mbuzi......"

Tuhuma za Lissu Mbowe hakuzitegemea..
Mbowe ni mkorofi hakuna sababu nyingine, temu hii alivyokabwa, kama anajua chama hicho kipo kwa minajiri ya chama cha CCM, nakuambia atasema temu hii

Ngoja abanwe kisawasawa maana kazoea kuwafanyia figisu wanaokuwa wakitaka nafasi hiyo
 
Mbowe huyu ambaye yuko mfukoni mwa Abdul au mwingi? Hii bishara ya mama Abdul na Sultan tunaifunga rasmi tarehe 21 January 2025
Watoto wadogo na washamba ndio mnamhusisha Mbowe na pesa za Abdul. Kwa taarifa yako Mbowe ni tajiri tangu Mwalimu Nyerere anafundisha Pugu Sekondari! Nini Abdul! Ahahahahaha!!!
 
Back
Top Bottom