Mbowe: Utawala wa Magufuli uliwatesa sana watu wa Kilimanjaro na Arusha!

Mbowe: Utawala wa Magufuli uliwatesa sana watu wa Kilimanjaro na Arusha!

Hii kauli ya Kiongozi huyu amekuwa akiirudia rudia sana naona kama haina afya kwa taifa!
Inabidi asamehe asonge mbele maisha ndo yalivyo! Yeye anaona utawala wa Magufuli uliwatesa lakini kuna watu hawaoni hivo!
Inabidi aondokane na hizi chembechembe za ubaguzi yeye kwanza!
Ni kauli ambayo hupendi kuisikia kwasababu haikufurahishi. Unapokuwa upande wa dhuluma , kwako ukweli ni MOTO unaounguza.

Ila yale yanayokufurahisha unaweza kuyasema WEWE mwenyewe.

Magufuli hawezi kuwa mbaya au dhalimu kwa kila jambo, ana mazuri yake pamoja na udhalimu wake.

Mapungufu yake lazima yasemwe ili kutengeneza kesho yenye mwanga.

Huwezi kujadili mafanikio bila kujadili changamoto ili kuboresha kesho yako.Ila angalia mafanikio yako yasimezwe na mapungufu yako.

USIOGOPE.
 
Anajificha kwenye haki huku anauchungu ndani yake mnafiki sana huyu mzee!
Penye haki HUWA haki inaonekana ikitendeka. Unapoona watu wanadai haki maana yake haitendeki , na km haki haitendeki maana yake Kuna wenye maumivu.

Ni kweli ana uchungu moyoni lkn amechagua msamaha na kutolipa kisasi. Na akasema hadharani.

Hakuna msamaha au maridhiano bila kuusema ukweli.
 
Mbaguzi alikuwa Magufuli. Yeye ndiye atubu kwanza
2015, watu wa asili ya Arusha na Kilimanjaro walikuwa wanahamasishana Tanzania nzima kumchagua Lowassa kwa sababu tu anatoka kanda yao , wakati huo huo wakina Tundu Lissu wametoka kutuimbisha wimbo kuwa Lowassa ni mmoja ya mafisadi papa nchini.
 
Wajaluo waliotoa Raisi wa Marekani na mirisasi Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Marekani Barak Obama mbona wametulia tu hawajidai wala hawana mbwembwe sembuse hicho kiaskari cheo cha chini makabila mengi yanatafuta fursa nje sema kelele.hawana kama wachaga
Ndio maana nasema wewe ni kiumbe wa ajabu kutokana na hoja zako.
Kwa mawazo yako Obama ni jaluo aliyekwenda Marekani kutafuta fursa?
Kama unafikiri hivyo hakuna njia jinsi ya kukusaidia kuelewa
 
Hitler aliishi nyakati ambazo hatukuwepo, lakini mpaka leo anajadiliwa.
Dah...
Mkuu Kama ungeusoma mkataba wa Versailles kati ya Dunia na Ujerumani.....Basi mjerumani yoyote mzalendo angeiingiza nchi vitani 🤣🤣🤣🤣🤭
 
Nyie endeleeni ku
Nyie endeleeni kuishi kwenye kijiji kikubwa cha Mbeya ndo maana hata Samia haji huko tokea aingie madarakani! Mnajifanyaga wajuaji mbele giza!
Nilidhani kijiji kidogo kumbe kikubwa na kinayashinda hadi majiji yako kwa mapato,viva kijiji kikubwa[emoji23]
 
Utawala uliwatesaje?

Kwamba Magufuli alikua anaua, anafunga na kuwapoteza watu wa Arusha na Kilimanjaro?

Kitu mbowe hana hua ni reasoning. Mbowe hutanguliza hisia kuliko uhalisia. Mbowe kuropoka lolote linalokuja kichwani mwake ni kawaida.

Magufuli aliwatesaje watu wa Kilimanjaro na Arusha?

Hii ni mara ya pili Mbowe anaendelea kusambaza chuki ya ukabila kwa wachaga wenzake. Mwaka jana alisema hili naona amerudia, sasa atalisema hili mara ngapi?

Hata kama kweli(ingawa sio kweli) Magufuli alifanya hivyo, Magufuli alishakufa mwaka mmoja uliopita, yeye sasa ajikite kwenye kujenga chama, Magufuli hayupo tena.

Sasa yeye kila akisimama tu kwa wachaga wenzake anamzungumzia Magufuli, Magufuli, Magufuli.

Magufuli angekua anawatesa na kuwachukia watu wa Kilimanjaro na Arusha angempa mkuu wa Usalama wake kutoka Kilimanjaro?

Wachaga na ukabila ni sawa na samaki na maji. Kabila la hovyo kabisa.

Vyama vingine ni vya kitapeli tu.
Kwani Magufuli akifa ndiyo watu wasiseme.
 
Waumini wa Magu wana wakati mgumu sana. mzee aliwajaza ujinga wa siasa za chuki sana. Sasa hivi wanakuwa na wakati mgumu kubadilika. Uchawa haulipi tena. Mama na mapungufu yake bado anaamini kwamba wote tunajenga Taifa Moja.

Siasa ni kama mapenzi. ukiziweka moyoni ipo siku utaumia tuu.
 
Haani nyinyi watu wa Mbeya hamna adhali yeyote kwenye serkali! Nyamazeni tu!
Nilidhani kijiji kidogo kumbe kikubwa na kinayashinda hadi majiji yako kwa mapato,viva kijiji kikubwa[emoji23]
 
CHADEMA kimekuwa chama cha ovyo sana. Ukabila unawaponza viongozi wa chama.
 
Mbowe anaongea ukweli pamoja na kwamba sio wachagga tu japo wengi ni wao issue ni kwamba aliwachukia wafanya biashara wakubw walio chuma awamu zilizopita akiamini wezi hivyo ukiongea wafanya biashara kundi kubwa ni wao.ukweli usemwe mwendazake amevunja rekodi.kwamambo ya kikatili.
Kweli walikuwa walikuwa wezi kwa kutolipa kodi na wengine walifungiwa mahesabu wakalipa.Sasa kosa lake ni lipi? Mfanyakazi analipishwa kodi kila mwezi kwa mshahara wa laki nne,yeye mfanyabiasha nani asilipe kodi tuwe tinajitambua na kufanya udadisi wakati wakuchangia hoja
 
Nani anasema tuliibiwa kura? Tunasema Magufuli alinajisi uchaguzi na hayo tuliona kwa macho yetu. Unatuokoteza vijimaneno vya jukwaani na kujifichia humo, ukidhani utauficha ukweli wa kilichotokea kwenye uchaguzi ule?
Labda mliibiwa huko kilimanjaro na arusha lakini kwa kanda ya ziwa mikoa ya kati na pwani hamna chenu mkajipang.
 
Arusha ndiyo sehemu ambako kiliporwa pesa nyingi kwenye maduka ya kubadilisha fedha kiliko eneo lolote la Tanzania. Mpaka leo, haijulikani pesa ile aliipeleka wapi, kwa maana hakuna mahali popote, si benki kuu wala wizara ya fedha, ilikopelekwa.
Una mimba ya miezi mingapi naona una hyperemesis gravidarum.
 
AAsante
Alisema ''.. Watu wa kaskazini watusubiri'' Rais wa nchi hawezi kutoa kauli ya kibaguzi kama hiyo
Hao wananchi wanakosa gani? Nini alichokiona na kutangaza mbele ya hadhara ?

Kukataa kupeleka maendeleo kwa watu wanaokusanya kodi ni ukataili na ubaguzi
Watetezi wa Magufuli hawaongelei rekodi yake mbaya sana ya kubomoa umoja wa kitaifa
Mijadala ya hovyo haikuwahi kutokea hadi pale Magufuli alipoingia madarakani na kupanda mbegu hii, lazima tikemee na rekodi yake iweke sawa.

Watu hawakuongea kwa simu, alirekodi kwa siri. Watu hawakuzungumzia chochote kwa kuogopa kupotezwa na wengi walipotea. Mfumo wa Watu wasiojulikana ume asisiwa na Magufuli aliwa na genge lake la akina Sabaya na Mkolomije . Rekodi ya Magufuli katika uhuru wa habari, wananchi n.k. ni mbaya. Tuweke rekodi yake sawa

Kwa ushahidi wa kauli yake ''... Nani angeshinda uchaguzi kama si mimi'' aliwaambia Wabunge. Kuharibika kwa mfumo wa Mahakama ni zao la Magufuli akiwata watoze watu faini badala ya kusimamia sheria. Mwendesha mashtaka akageuka kuwa TRA. Tuweke rekodi yake sawa

Tunaambiwa kajenga barabara, SGR n.k. Vitu hivyo alijenga Nyerere

Tumeambiwa anatumia pesa za ndani, leo tunajua tuna madeni makubwa ya Taifa

Rekodi ya Magufuli katika utu ni ya kujiuliza. Watu wanaokotwa bharini, kwenye mifereji tunaambiwa wametoka South Africa.

Uwepo wa Genge la Sabaya na Makonda na wasiojulikana ni zao la Magufuli.

Pesa za kununua ndege hazikupitia mfumo wa nchi, hatujui zimetumikaje akishirikiana na mtoto wa dada yake. Magufuli aligeuza hazina kama mali binafsi.
Aliua taasisi kama vyombo vya habari, Bunge na idara nyingine muhimu za nchi.

Tuweke rekodi sawa!

JokaKuu
Asante Nguruvi3 kwa kukoleza mada
 
Dawa ni kuiondoa CCM ndo imezaa haya yote.
Kilichopo hapa ni kupigania iondoke tu tupumue
 
Back
Top Bottom