Alisema ''.. Watu wa kaskazini watusubiri'' Rais wa nchi hawezi kutoa kauli ya kibaguzi kama hiyo
Hao wananchi wanakosa gani? Nini alichokiona na kutangaza mbele ya hadhara ?
Kukataa kupeleka maendeleo kwa watu wanaokusanya kodi ni ukataili na ubaguzi
Watetezi wa Magufuli hawaongelei rekodi yake mbaya sana ya kubomoa umoja wa kitaifa
Mijadala ya hovyo haikuwahi kutokea hadi pale Magufuli alipoingia madarakani na kupanda mbegu hii, lazima tikemee na rekodi yake iweke sawa.
Watu hawakuongea kwa simu, alirekodi kwa siri. Watu hawakuzungumzia chochote kwa kuogopa kupotezwa na wengi walipotea. Mfumo wa Watu wasiojulikana ume asisiwa na Magufuli aliwa na genge lake la akina Sabaya na Mkolomije . Rekodi ya Magufuli katika uhuru wa habari, wananchi n.k. ni mbaya. Tuweke rekodi yake sawa
Kwa ushahidi wa kauli yake ''... Nani angeshinda uchaguzi kama si mimi'' aliwaambia Wabunge. Kuharibika kwa mfumo wa Mahakama ni zao la Magufuli akiwata watoze watu faini badala ya kusimamia sheria. Mwendesha mashtaka akageuka kuwa TRA. Tuweke rekodi yake sawa
Tunaambiwa kajenga barabara, SGR n.k. Vitu hivyo alijenga Nyerere
Tumeambiwa anatumia pesa za ndani, leo tunajua tuna madeni makubwa ya Taifa
Rekodi ya Magufuli katika utu ni ya kujiuliza. Watu wanaokotwa bharini, kwenye mifereji tunaambiwa wametoka South Africa.
Uwepo wa Genge la Sabaya na Makonda na wasiojulikana ni zao la Magufuli.
Pesa za kununua ndege hazikupitia mfumo wa nchi, hatujui zimetumikaje akishirikiana na mtoto wa dada yake. Magufuli aligeuza hazina kama mali binafsi.
Aliua taasisi kama vyombo vya habari, Bunge na idara nyingine muhimu za nchi.
Tuweke rekodi sawa!
JokaKuu