Jitahidi kuvumilia ukweli hata kama unauma. Aliyekuwa anafanya huo uhayawani mliona yuko sawa, kwanini hamkumwambia matendo yake hayana afya kwa taifa?
Ni ukweli usiofichika Magufuli alwachukia sana na watu wa Kilimanjaro na Arusha
Chuki yake ilipitiliza kiasi cha kutamka akiwa Iringa ''....watu wa kaskazini sasa watusubiri''
Akapanda chuki nyingine watu wa kanda ya ziwa wakisema ''...ni zamu yetu''
Legacy ya Magufuli ni pamoja na kuvunja umoja wa kitaifa, kupanda mbegu za kikanda, kikabila na kuendekeza udini.
Marehemu Mkapa alimwambia kidiplomasia kupitia kitabu chake kwamba, alipomwambia Nyerere nani awe katika baraza lake Mwl alimjibu hatamshauri, isipokuwa atambue nchi ina makabila na dini tofuati na hilo azingatie. Magufuli hakuzingatia
Kile kinachoitwa ''kutumbua majibu' kilikuwa kiini macho tu, Magufuli alilenga makabila na dini na baada ya kumaliza hatukusikia tena kutumbua.
Katika watu waliojaribu sana kuvunja umoja wa kitaifa , mshikamano na upendo Magufuli alikuwa kiongozi wao, hilo lisemwe bila haya wala soni.
Kwasababu ya legacy yake hutawasikia watu wakizungumzia mambo kadhaa ikiwemo rekodi ya Utu, haki, utawala wa sheria, demokrasia, uhuru wa wananchi n.k. Utawasikia wetetezi wakizungumzia kajenga flyover n.k. kuficha madhaifu yake
Kwa miaka zaidi ya 20 Nyerere anachambuliwa , ni haki kumchambua Magufuli kwa mema na mabaya yake, si kutueleza flyover .
Pascal Mayalla JokaKuu