Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho


Swali la kijinga.

Hivi hata ukiwa ni wewe umeingia bungeni, ukakuta mshahara ni huo, utaacha kuupokea? Na ukiuacha itasaidia nini?

Lakini ukiingia huko, ukakuta mshahara ni huo, na ukaona kwa kuzingatia uhalisia wa nchi, siyo halali. Ukautangazia umma kwa uwazi, tayari umetimiza wajibu wako. Wanaotakiwa kuchukua hatua ni wenye pesa yao, ambao ni wananchi. Kama wao wanaona ni halali mbunge achukue 26m kwa mwezi na Rais 50m kwa mwezi, basi hakuna wakubadilisha.
 
Acha mpigwe tu,subiri foleni uchafue kidole na wino uwachague tena

Ova
 

Kweli PESA ni fitna asee jamaa angu.

huyu jamaa kipindi ni mbunge alikuwa sio wenge Sana.

CCM mrudisheni huyu jamaa bungeni
 
Kuna kipindi Wabaguzi wa rangi huwa wanasema Mwafrika Mweusi hawezi kujitawala,huwa nawapinga sana lakini kwa mbali huwa najisemea kwenye Nafsi yangu kuwa huenda wanasema ukweli.
 
Na katika hali hii kima cha chini cha pensheni kwa wastaafu imebaki kuwa Tshs. 100,000/= kwa mwezi tangu utawala ya Kikwete 2015 - miaka 9 iliyopita. Tunaambiwa eti wataalam wanaangalia hesabu za mifuko ya pensheni kuona kama kuna uwezekano wa kufanya mabadiriko, ambayo kiutaratibu yanatakiwa kutekelezwa kila baada ya miaka mitatu. Mungu ibariki Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…