Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Mbowe: Wabunge wamejiongezea Mishahara Kutoka Tsh milioni 13 za awali na sasa wanalipwa Tsh milioni 18 kwa mwezi mbali na posho

Itakuja hapa misukule akina choice variable na MamaSamia2025 kusifia ujinga na ufisadi wa maCCM. Majitu kama haya bora yafe tu!
Mbowe kaongea kitu sahihi ila kinafiki sana kwasababu inamuuma kuwa nje ya bunge. Ninatumaini uchaguzi 2025 utakuwa huru na wa haki ili nao waingie bungeni kutafuna keki ya nchi. Wabunge huwa kitu kimoja bila kujali vyama linapokuja suala la maslahi yao.
 
Wakati ule akiwa bungeni alikuwa anapokea hiyo milioni 13 na yeye????? au hakukubali kupokea? Maana hakuna mkutano wowote aliwahi kusimama wakati ule na yeye ni mbunge akalalamika kuwa analipwa hela nyingi mno zipunguzwe.

Porojo za wanasiasa baaana!😆
 
Manufaa ya tozo. Hapo lazima fisi wa CCM waliojazana bungeni wasifie tozo za Samia na Mwigulu maana faida yake wanaiona.

Kwa tozo tu za sasa wamepanda mpaka Tsh 26m kwa mwezi (mshahara 18m + posho 8m). Samia akiongeza tozo nyingine, watapanda mpaka angalaoTsh 35m kwa mwezi. Hawa lazima waombe Samia awe Rais wa maisha.

Hii ndiyo maana iliyokusudiwa na Samia kuwa kila mmoja ale kwa urefu wa kamba yake.
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Bunge la JMT wamejiongezea Mishahara kutoka TSH 13 million walizokuwa wanalipwa awali hadi TSH 18 million

Mbowe amesema mshahara huo ni mbali na Posho mbalimbali wanazolipwa kila Siku

Jumaa Mubarak 😀🔥

----
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amedai kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamejiongezea mishahara yao kutoka milioni 13 waliyokuwa wanapata hapo awali hadi kufikia milioni 18 kwa mwezi, hiyo ikiwa ni nje ya posho ya vikao anayopatiwa Mbunge kila anapohudhuria kikao kimoja cha Bunge

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Machi 21.2024 Babati mjini, mkoani Manyara Mbowe amesema kuwa mara nyingi viongozi wa serikali wamekuwa wakijitokeza hadharani na kueleza kuwa uchumi umekua hapa nchini, jambo ambalo anakubaliananalo kwa kutumia kipimo cha pato la Taifa (GDP) lakini ameeleza kuwa uchumi huo umekua kwa watu wachache walioko serikalini na sio kwa mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla wake

Amesema viongozi walioko serikalini wamekuwa wakiendekeza maisha ya anasa ambayo kwa kiasi kikubwa hayaangalii maslahi ya nchi na wananchi wake ndio maana inawawia vigumu kukubali kufanya marekebisho ya msingi ya sheria za nchi kutokana na msingi wa uwepo wa Katiba mpya

Ametolea mfano kupitishwa kwa sheria ya mafao ya wenza wa viongozi kama sehemu ya anasa hizo kwa kuwa sasa mwenza wa Rais mstaafu analazimika kupokea asilimia 60 ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani, wakati Rais mstaafu akipokea asilimia 80 ya mshahara huo, hiyo ikienda sambamba na kupatiwa magari yanayobadilishwa kila baada ya muda, walinzi, nyumba na watumishi wengine binafsi.

Chanzo: Jambo Tv
Ana hoja ya msingi haya ndio mambo ya kuwaletea wananchi wafanye maamuzi yao na kuihoji serikalai yao
 
Back
Top Bottom