The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania(TCD) Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema wamekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na serikali lakini makubaliano ya majadiliano hayo yamekuwa hayatekelezwi.
Pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano huo kuwaomba CHADEMA kukaa na serikali kujadili kwa pamoja ili kufikia maridhiano pasipo kuandamana lakini Mbowe amesema watazungumza na pia wataandamana “wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana lakini haina maana kwamba hatutazungumza tutazungumza tu, namna ambavyo wanajiandaa wao kutuua na sisi huenda tunajiandaa kufa”
Mbowe amezungumza hayo wakati akifunga siku ya kwanza ya mkutano wa TCD na wadau wakifanya Tathmini ya hali ya demokrasia nchini ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani ambapo yanafanyika kwa siku mbili Septemba 19 na Septemba 20 kesho.
Huu ndiyo uongozi kusimamia kile kilicho sahihi na unachokiamini
===========================================
UPDATES
Na wakati huohuo Marekani kupitia kwa Balozi wake nchini Tanzania Mr Michael Battle amepingana vikali na waziwazi na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na kusema katika hotuba ya kali kabisa aliyoitoa katika kongamano hilo la TCD...
Amesema, "Marekani imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo na demorasia ktk Tanzania kwa kiasi na kwa kwa hiyo USA haiwezi kukaa kimya kuona watu wakiuwawa na kutekwa bila serikali ya Tanzania kuchukua hatua dhabiti kukomesha hali hii...."
Mtazame na msikilize👇🏻👇🏻
#SAMIA MUST GO.......
Pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano huo kuwaomba CHADEMA kukaa na serikali kujadili kwa pamoja ili kufikia maridhiano pasipo kuandamana lakini Mbowe amesema watazungumza na pia wataandamana “wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana lakini haina maana kwamba hatutazungumza tutazungumza tu, namna ambavyo wanajiandaa wao kutuua na sisi huenda tunajiandaa kufa”
Mbowe amezungumza hayo wakati akifunga siku ya kwanza ya mkutano wa TCD na wadau wakifanya Tathmini ya hali ya demokrasia nchini ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani ambapo yanafanyika kwa siku mbili Septemba 19 na Septemba 20 kesho.
- Soma Pia
Mbowe: Mtu wa kwanza kuwajibishwa kwenye matukio ya utekaji ni Rais Samia. CHADEMA kuanza kampeni ya 'Samia Must Go'
News Alert: - Polisi yapiga marufuku maandamano ya CHADEMA yasema ni haramu. Yasema chama hicho kimekuwa kikipanga mikakati ya kuchochea vurugu