Mbowe: wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana. Namna ambavyo wanajiandaa wao kutuua na sisi huenda tunajiandaa kufa

The Palm Beach

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
1,967
Reaction score
4,267
Mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania(TCD) Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema wamekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na serikali lakini makubaliano ya majadiliano hayo yamekuwa hayatekelezwi.

Pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano huo kuwaomba CHADEMA kukaa na serikali kujadili kwa pamoja ili kufikia maridhiano pasipo kuandamana lakini Mbowe amesema watazungumza na pia wataandamana “wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana lakini haina maana kwamba hatutazungumza tutazungumza tu, namna ambavyo wanajiandaa wao kutuua na sisi huenda tunajiandaa kufa”

Mbowe amezungumza hayo wakati akifunga siku ya kwanza ya mkutano wa TCD na wadau wakifanya Tathmini ya hali ya demokrasia nchini ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani ambapo yanafanyika kwa siku mbili Septemba 19 na Septemba 20 kesho.

Huu ndiyo uongozi kusimamia kile kilicho sahihi na unachokiamini
===========================================
UPDATES
Na wakati huohuo Marekani kupitia kwa Balozi wake nchini Tanzania Mr Michael Battle amepingana vikali na waziwazi na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na kusema katika hotuba ya kali kabisa aliyoitoa katika kongamano hilo la TCD...

Amesema, "Marekani imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo na demorasia ktk Tanzania kwa kiasi na kwa kwa hiyo USA haiwezi kukaa kimya kuona watu wakiuwawa na kutekwa bila serikali ya Tanzania kuchukua hatua dhabiti kukomesha hali hii...."

Mtazame na msikilize👇🏻👇🏻

#SAMIA MUST GO.......
 
Mwenyekiti wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania(TCD) Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema wamekuwa na majadiliano ya mara kwa mara na serikali lakini makubaliano ya majadiliano hayo yamekuwa hayatekelezwi.

Pamoja na wadau mbalimbali katika mkutano huo kuwaomba CHADEMA kukaa na serikali kujadili kwa pamoja ili kufikia maridhiano pasipo kuandamana lakini Mbowe amesema watazungumza na pia wataandamana “wanaokusudia kuandamana wana hasira na wataandamana lakini haina maana kwamba hatutazungumza tutazungumza tu, namna ambavyo wanajiandaa wao kutuua na sisi huenda tunajiandaa kufa”

Mbowe amezungumza hayo wakati akifunga siku ya kwanza ya mkutano wa TCD na wadau wakifanya Tathmini ya hali ya demokrasia nchini ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani ambapo yanafanyika kwa siku mbili Septemba 19 na Septemba 20 kesho.

Huu ndiyo uongozi kusimamia kile kilicho sahihi na unachokiamini
#SAMIA MUST GO.......
Abwabahe na kuhororoja apendavyo, polisi wameswma "maandamano ni narufuku".

Alete wanawe na yeye mwenyewe waongoze maandamno wawe wa mwanzo kuchezea mkong'oto wa FFU.

Siyo kusukumia watoto za watu tu wachezee mkong'oto.
 
Na kumshikilia Boni ndio kunaongezea watu hasira.
Hakuna kurudi nyuma Hizi siasa za ulaghai zinazofanywa na watawala, hazikubaliki hata kidogo. Maandamano ndiyo njia sahihi ya wazi kuthibitisha hisia walizo nazo wananchi. Polisi wajiandae kusimamia maandamano kama sheria inavyotaka. Kama hawana muda, kwa sababu wapo busy na utekaji, wautaarifu umma ili umma ujisimamie wenyewe.
 
Back
Top Bottom