Mbowe: Watanzania ni Wavivu na Waoga. Wanataka kila kitu afanye Tundu Lissu au Mbowe, hatutafika kwa utaratibu huu!

Na huo ndiyo ujinga anaosema Mbowe wa kusubiri kila jambo lifanywe na Lissu au Mbowe! Hivi hao wakisamaratishwa hapo mtabaki na nani? Chama hakijiwezi kabisa hiki!
 
Haifai kwenye nn
Impunity, kitendo cha mfumo mzima wa utoaji haki (judicial system) kutokuwa huru kina athari za moja kwa moja mpaka kwa raia.
Kwa mfano, hivi kama mahakama zingekuwa huru kuna polisi angebambikia mtu kesi? Kina Sabaya wangechukua mali za watu kibabe?
 
Bora amekiri mwenyewe.chadema haiwezi kubadili chochote kwenye nchi hii.mbowe na lisu wameshindwa wanatafuta namna yakuwasukumizia zigo wananchi.wanataka raia waingie lod kuandamana kudai katiba mpya?
 
Ukweli mchungu sana
 
Mbowe endelea na biashara zako. Tanzania ipo salama chini ya Samia Suluhu, mwenyewe umekiri hili mara kadhaa

Katiba ya wananchi itapatikana kupitia popular movement ya wananchi na sio vikao vya Ikulu
We ni mninga tu
 
Ila una uhakika hao wananchi hitaji lao ni katiba mpya ila wanaogopa kuidai?

Kumbe. Huoni hata umeme unakatika na hawana uwezo wa kushinikiza upatikane wakati wanalipia hiyo huduma, na ndio unaoendesha shughuli zao?
 
Sijaelewa tafsiri ya uoga ni ipi. Tutofautishe uoga na ukorofi, sasa ikiwa wananchi hawana imani na wanasiasa ni vipi unaweza kuwashawishi waingie barabarani.
 
Impunity, kitendo cha mfumo mzima wa utoaji haki (judicial system) kutokuwa huru kina athari za moja kwa moja mpaka kwa raia.
Kwa mfano, hivi kama mahakama zingekuwa huru kuna polisi angebambikia mtu kesi? Kina Sabaya wangechukua mali za watu kibabe?

Hata katiba mpya ikija unadhani watu wa Aina hiyo hawatakuwepo ?

Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu Kuchukua mali ya mtu mwingine kiholela?

Katiba mpya haina suluhisho Kwa hili trust me

Coz still ni watu ndio watakaa kwenye mahakama na sio katiba
 
Hata katiba mpya ikija unadhani watu wa Aina hiyo hawatakuwepo ?
Watakuwepo, na ndio maana tunadai iwepo katiba ambayo itatoa uhuru kamili wa mfumo wa utoaji haki. Ili kuwadhibiti watu wa namna hiyo kupitia fair orders za mahakama.
Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu Kuchukua mali ya mtu mwingine kiholela?
Technically inaruhusu. kwa sababu kinachotakiwa, na kinachoweza kulinda raia na mali zao ni Sheria tuu na sio jeshi la polisi kama ilivyo sasa.
Katiba mpya haina suluhisho Kwa hili trust me
suluhisho litapatikana endapo tuu, uelewa na utayari wa wananchi kudai mabadiliko ya kikatiba (whether marekebisho ya hii ya 77 au nyingine mpya) utakuwa wa kiwango cha kuridhisha kuliko ilivyo mpaka sasa.
Coz still ni watu ndio watakaa kwenye mahakama na sio katiba
Mwisho, asilimia kubwa ya watu wanafanya uovu kwa kuangalia weaknesses kwenye sheria zilizopo tayari.
 
Amesahau hadi leo kua kuna wananchi wapo kifungoni,wengine mayatima ,wengine walemavu kwa madhira ya kukipambania chama?Sio hao tuliowachagua WAKAANZA KUUNGA MKONO JUHUDI AWAMU YA TANO, aache upumbavu na sio kuanza kudharau wananchi baada ya kua na UHAKIKA wa KULAMBA ASALI JUMBA JEUPE
 
Pweinti

Mtu anachaguliwa akiwa Chadema halafu akihaidiwa cheo CCM anaunga juhudi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…