Mbowe: Watanzania ni Wavivu na Waoga. Wanataka kila kitu afanye Tundu Lissu au Mbowe, hatutafika kwa utaratibu huu!

Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema Watanzania ni Wavivu wanategemea kila kitu afanye Tundu Lisu na Mbowe

Kwa utaratibu huu hata Katiba mpya itakuwa ngumu kuupata, amesema

Wananchi ni lazima mtumie WINGI wenu kuibana Serikali itekeleze matarajio yenu vinginevyo mtaendelea Kuwa Walalamikaji wa kudumu, amesisitiza Mbowe katika mkutano wa hadhara Temeke
Fanyeni nyie maana Nyerere alifanya mbona? 😀😀😀😀..

Hii Nchi haijajengwa Kwa misingi ya vurugu so msitegemee kutumia hiyo njia kwamba itawasaidia,haitakaa itokee nikaandamane wakati Watoto wa Lisu na Mbowe wako ulaya.
 
Haya maneno nusu nusu ya kuokoteza huwa unayaleta huku kwa manufaa ya CCM yako, ila yale mengine yanayokuwepo kwenye hotuba husika unayakwepa makusudi kwa sababu ya uoga wako.

Unaonesha kama vile Mbowe amekata tamaa kitu ambacho sio kweli, ndio kwanza wana mipango mipya itakayowawezesha ili kuyafikia malengo waliyojiwekea.

Mfano Mbowe amesema, watatengeneza vijana elfu moja kila mkoa ili wawe walimu.wa kuhamasisha upatikanaji wa Katiba Mpya, hili hujalisema!.
Hao Vijana buku tukiwabaini tuu watatafuta Nchi Yao🤸🤸
 
Kwa taarifa yako ili anayodai Mbowe yatimizwe, ni lazima Lisu awepo. Hiyo itapelekea kuona madai ya Lisu ya mabavu hatayapata, ila wataona aibu mbona hata ya Mbowe anayoyadai kiungwana bado hawayatoi? Hapo ni aidha wakubali ya Lisu ya mabavu, au ya Mbowe ya kiungwana. Hivyo tu Boss.
Kumbe mnalenga kufanya Nchi isitawalike? Tunawasubiria
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema Watanzania ni Wavivu wanategemea kila kitu afanye Tundu Lisu na Mbowe

Kwa utaratibu huu hata Katiba mpya itakuwa ngumu kuupata, amesema

Wananchi ni lazima mtumie WINGI wenu kuibana Serikali itekeleze matarajio yenu vinginevyo mtaendelea Kuwa Walalamikaji wa kudumu, amesisitiza Mbowe katika mkutano wa hadhara Temeke
Kwani wao sio waTz mbona enzi zile waliufyata.
Kweli leo anafokea wa TZ
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Mbowe amesema Watanzania ni Wavivu wanategemea kila kitu afanye Tundu Lisu na Mbowe

Kwa utaratibu huu hata Katiba mpya itakuwa ngumu kuupata, amesema

Wananchi ni lazima mtumie WINGI wenu kuibana Serikali itekeleze matarajio yenu vinginevyo mtaendelea Kuwa Walalamikaji wa kudumu, amesisitiza Mbowe katika mkutano wa hadhara Temeke
Hapo Mbowe amegonga penyewe !!
 
Watakuwepo, na ndio maana tunadai iwepo katiba ambayo itatoa uhuru kamili wa mfumo wa utoaji haki. Ili kuwadhibiti watu wa namna hiyo kupitia fair orders za mahakama.

Technically inaruhusu. kwa sababu kinachotakiwa, na kinachoweza kulinda raia na mali zao ni Sheria tuu na sio jeshi la polisi kama ilivyo sasa.

suluhisho litapatikana endapo tuu, uelewa na utayari wa wananchi kudai mabadiliko ya kikatiba (whether marekebisho ya hii ya 77 au nyingine mpya) utakuwa wa kiwango cha kuridhisha kuliko ilivyo mpaka sasa.

Mwisho, asilimia kubwa ya watu wanafanya uovu kwa kuangalia weaknesses kwenye sheria zilizopo tayari.

Hata katiba ya sasa inatoa uhuru mkubwa Kwa mahakama

Kama watu wanavunja sheria Kwa katiba hii then hata hiyo mpya katiba itavunjwa Tu na hakuna kitu mtafanya

Sometimes mnaongea kama mko ulaya au Marekani mnasahau kwamba hapa ni Africa

Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu kuiba? Na je watu hawaibi? Hiyo katiba mpya itazuia nn hao watu kuiba?
 
Pengine katiba iliyopo haikupewa meno thabiti ya kung’ata pale inapovunjwa ndio maana inatakiwa ije ile itakayokuwa na meno ya kung’ata kweli kweli !!
 
Katiba mpya na lazima, hiyo siku ukae mbele we na mkeo utuzuie, na vyombo vya dola vikae pembeni.

Wasituletee ujinga,wanataka tuwapambanie wao ,,siasa ni kazi wapambane na familia zao,kila siku analia kua kapoteza. MABILIONI ya pesa ,,je hao waliopoteza baba ,mama kwa ajili ya siasa!!kweli ndo maana ukaitwa DJ
 
Pengine katiba iliyopo haikupewa meno thabiti ya kung’ata pale inapovunjwa ndio maana inatakiwa ije ile itakayokuwa na meno ya kung’ata kweli kweli !!

As long as wahusika ni watu, tena watu wenyewe ni waafrica, I'm telling you, katiba mpya haitokuja na jipya lolote

Labda kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa hapo sawa
 
Hata katiba ya sasa inatoa uhuru mkubwa Kwa mahakama
"Uhuru mkubwa" hautoshi, inatakiwa uhuru kamili.
Kama watu wanavunja sheria Kwa katiba hii then hata hiyo mpya katiba itavunjwa Tu na hakuna kitu mtafanya
Ndiyo itavunjwa tunajua, ila uwajibikaji utakuwepo kwani mahakama itakuwa na mamlaka ya kulinda na kusimamia misingi ya sheria mama, na sheria nyingine ndani na nje ya nchi.
Sometimes mnaongea kama mko ulaya au Marekani mnasahau kwamba hapa ni Africa
Tofauti ya Africa na huko kwingine kunatengenezwa na aina ya sheria za hovyo za Afrika, zikibadilika tutakuwa kwenye mzani sawa katika masuala mbalimbali muhimu.
Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu kuiba? Na je watu hawaibi? Hiyo katiba mpya itazuia nn hao watu kuiba?
Inaruhusu baadhi ya watu kuiba, na wanaiba. Katiba mpya haitazuia mtu kuiba kwakuwa siyo 'password ya kuingia sehemu fulani' ila wezi watawajibika ipasavyo.
 
As long as wahusika ni watu, tena watu wenyewe ni waafrica, I'm telling you, katiba mpya haitokuja na jipya lolote

Labda kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa hapo sawa
Duh ! Kwahiyo tufanyeje ?! Yaani ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu ?!
 
"Uhuru mkubwa" hautoshi, inatakiwa uhuru kamili.

Ndiyo itavunjwa tunajua, ila uwajibikaji utakuwepo kwani mahakama itakuwa na mamlaka ya kulinda na kusimamia misingi ya sheria mama, na sheria nyingine ndani na nje ya nchi.

Tofauti ya Africa na huko kwingine kunatengenezwa na aina ya sheria za hovyo za Afrika, zikibadilika tutakuwa kwenye mzani sawa katika masuala mbalimbali muhimu.

Inaruhusu baadhi ya watu kuiba, na wanaiba. Katiba mpya haitazuia mtu kuiba kwakuwa siyo 'password ya kuingia sehemu fulani' ila wezi watawajibika ipasavyo.
Umemaliza mchezo ! Maelezo sahihi kabisa 👍🙏
 
2023 alisema anastaafu uenyekiti mbona naona kama hakuna dalili ya kustaafu
 
Back
Top Bottom