Mbowe: Watanzania ni Wavivu na Waoga. Wanataka kila kitu afanye Tundu Lissu au Mbowe, hatutafika kwa utaratibu huu!

Fanyeni nyie maana Nyerere alifanya mbona? 😀😀😀😀..

Hii Nchi haijajengwa Kwa misingi ya vurugu so msitegemee kutumia hiyo njia kwamba itawasaidia,haitakaa itokee nikaandamane wakati Watoto wa Lisu na Mbowe wako ulaya.
 
Hao Vijana buku tukiwabaini tuu watatafuta Nchi Yao🤸🤸
 
Kumbe mnalenga kufanya Nchi isitawalike? Tunawasubiria
 
Kwani wao sio waTz mbona enzi zile waliufyata.
Kweli leo anafokea wa TZ
 
Hapo Mbowe amegonga penyewe !!
 
Hata katiba ya sasa inatoa uhuru mkubwa Kwa mahakama

Kama watu wanavunja sheria Kwa katiba hii then hata hiyo mpya katiba itavunjwa Tu na hakuna kitu mtafanya

Sometimes mnaongea kama mko ulaya au Marekani mnasahau kwamba hapa ni Africa

Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu kuiba? Na je watu hawaibi? Hiyo katiba mpya itazuia nn hao watu kuiba?
 
Pengine katiba iliyopo haikupewa meno thabiti ya kung’ata pale inapovunjwa ndio maana inatakiwa ije ile itakayokuwa na meno ya kung’ata kweli kweli !!
 
Katiba mpya na lazima, hiyo siku ukae mbele we na mkeo utuzuie, na vyombo vya dola vikae pembeni.

Wasituletee ujinga,wanataka tuwapambanie wao ,,siasa ni kazi wapambane na familia zao,kila siku analia kua kapoteza. MABILIONI ya pesa ,,je hao waliopoteza baba ,mama kwa ajili ya siasa!!kweli ndo maana ukaitwa DJ
 
Pengine katiba iliyopo haikupewa meno thabiti ya kung’ata pale inapovunjwa ndio maana inatakiwa ije ile itakayokuwa na meno ya kung’ata kweli kweli !!

As long as wahusika ni watu, tena watu wenyewe ni waafrica, I'm telling you, katiba mpya haitokuja na jipya lolote

Labda kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa hapo sawa
 
Hata katiba ya sasa inatoa uhuru mkubwa Kwa mahakama
"Uhuru mkubwa" hautoshi, inatakiwa uhuru kamili.
Kama watu wanavunja sheria Kwa katiba hii then hata hiyo mpya katiba itavunjwa Tu na hakuna kitu mtafanya
Ndiyo itavunjwa tunajua, ila uwajibikaji utakuwepo kwani mahakama itakuwa na mamlaka ya kulinda na kusimamia misingi ya sheria mama, na sheria nyingine ndani na nje ya nchi.
Sometimes mnaongea kama mko ulaya au Marekani mnasahau kwamba hapa ni Africa
Tofauti ya Africa na huko kwingine kunatengenezwa na aina ya sheria za hovyo za Afrika, zikibadilika tutakuwa kwenye mzani sawa katika masuala mbalimbali muhimu.
Kwani katiba ya sasa inaruhusu mtu kuiba? Na je watu hawaibi? Hiyo katiba mpya itazuia nn hao watu kuiba?
Inaruhusu baadhi ya watu kuiba, na wanaiba. Katiba mpya haitazuia mtu kuiba kwakuwa siyo 'password ya kuingia sehemu fulani' ila wezi watawajibika ipasavyo.
 
As long as wahusika ni watu, tena watu wenyewe ni waafrica, I'm telling you, katiba mpya haitokuja na jipya lolote

Labda kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa hapo sawa
Duh ! Kwahiyo tufanyeje ?! Yaani ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu ?!
 
Umemaliza mchezo ! Maelezo sahihi kabisa 👍🙏
 
2023 alisema anastaafu uenyekiti mbona naona kama hakuna dalili ya kustaafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…