Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

Mbuge Flatei Massay apiga sarakasi Bungeni kuonesha kulalamika kuhusu ahadi anazopewa kila mara bila kutekelezwa, afanya marejeo ya sauti za mawaziri

goroko77

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
8,845
Reaction score
13,072
Mbuge wa Mbulu ameoneshwa kukerwa hadi kuamua kupiga sarakasi bungeni bila kujali uwepo wa spika

Ni sawa mmbuge kupiga sarakasi au mweleka kuonesha kukerwa na ahadi zizizo tekelezeka?

===

Kuruka sarakasi kwa mbunge Flatei ni jambo analotamani kulifanya mara nyingi, Mei 17, 2021 pia alipokuwa akilalamikia matatizo ya jimboni kwake aliomba kuruka sarakasi ili kuonesha kuwa ametumwa na wananchi wake kuwasemea.

Kabla ya kuruka sarakasi, Mbunge huyo wa Mbulu alifanya marejeo kwenye kishkwambi chake ya sauti zilizorekodiwa za waziri wa ujenzi na naibu wake wakitoa ahadi kwenye vikao vya Bunge vilivyopita za kukamilisha ujenzi wa barabara Mbulu jambo ambalo halijatimizwa hadi sasa.

Sarakasi.jpg


Pia soma: Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay almanusura kupiga sarakasi Bungeni ili ajengewe barabara jimboni

 
Kwani huyu hawezi kuleta hoja yake bungeni mpaka abinuke sarakasi.

Tutafsiri kuwa ni ushujaa ama upumbavu..!
 
hii nchi sasa dharau zimezidi kipimo,

huku ni kulinajisi bunge tukufu, huyu ashughulikiwe na kamati ya nidhamu,

hivi hawa wabunge wameokotwa wapi, hivi vitu hata mtoto wa secondary hafanyi

ccm ijitafakari tumechoka kuletewa machizi halafu yanapitishwa kinguvu na tume

upumbavu mtupu
 
Wangempa kibarabara aruke nyingi kabisa... halafu mwandishi hiyo siyo samasoliti usitudanganye
 
Back
Top Bottom