Mbunge Abbas Tarimba apendekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu ili magari yao yatambulike barabarani

watukuja na kudai awe anasindikizwa na trafik ili awatumikie vizuri wananchi wake!
 
Tunawabunge wabinafsi sana.Yani mamilion ya hela wanayolipwa kwa kazi ya kusifia seriksli na rais hayawatoshi wanataka umaarufu zaidi???
 
Namshauri bwana tarimba wabunge pia wawe na MAKABURI MAALUM ili wakifa WASIOZE
 
Mbunge wa Kinondoni Abasi Tarimba amesema suala la Wabunge kupeperusha bendera kwenye magari yao ni gumu kwa baadhi ya Wabunge akitolea mfano Wabunge wa Dar es salaam ambapo amependekeza watengenezewe namba maalum ambazo zitasaidia kuwahi katika kutekeleza majukumu yao na pia kurahisisha kutambulika wanapokuwa katika misafara ya kiserikali .

Tarimba ameyasema hayo Bungeni leo June 11, 2025 wakati akichangia hoja katika taarifa ya Kamati ya Kanuni za Bunge ambapo amesema “Kuna Wabunge ambao tunatoka katika Mikoa ambayo hatuwezi tukapeperusha bendera kwa mfano Wabunge wa Dar na naamini hata tukiwepo Dodoma hatupeperushi bendera na tukienda Zanzibar hatuwezi kupeperusha bendera sasa inatokea wakati kuna misafara ya kitaifa na kimkoa ambapo tunatakiwa tufike maeneo fulani kwa uharaka au saa nyingine tunakuwepo kwenye ile misafara

Kwakuwa magari yetu yanakuwa hayana utambulisho wowote ule, tunajikuta katika ile orodha ya Watu ambao tuko kwenye msafara gari lako linawekuwa nyuma kisi kwamba ukiitwa Mbunge utoe salamu ndio kwanza unatafuta sehemu ya kupark sasa nilikuwa nafikiria kwamba Bunge haliwezi likafikiria tukawa na namba ya utambulisho ya gari (Plate Number) malumu kwa ajili ya Wabunge"
 
Uyu mzee akirudi tena bungeni baada ya uchaguzi nitashangaa sana hata kwa wana ccm wenyewe aisee magu aliwapa watu wa ajabu sana ubunge
 
Kwanza hatumtaki jimboni huyo spika kama anamtaka ampeleke jimboni kwake akawakilishe.

Sisi huku tunamleta kijana mdogo tu machachari
 
Anauthibitisha uponjoro wake sasa😄, kichwa kipo kipo full betting tips😂😂. Watueleze tuendelee kutekwa huku nje na wao wakae kimya kama kawaida yao na baadae waje kutuomba tuwapigie kura
 
Tanzania tulikoseaa wapi..tunaludi nyuma..badala ya kwenda mbele
 
Sifa tuuuuu, hapa hamna kitu kumbe

Napendekeza wabunge wawe masikini labda itasaidia, yaani tajiri asiruhusiwe hata kugombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…