Mbunge Abbas Tarimba apendekeza wabunge wapewe 'plate number' maalumu ili magari yao yatambulike barabarani

Ponjoro wa Kinondoni.
No Reforms No Elections.
 
Ndio vizuri ili kikinuka mnakuwa mnajua nani ni nani huko barabarani.
 
Ponjoro mkubwa kabisaaaa!
 
Mbunge Tarimba amesahau kwamba Ubunge una ukomo, na ukomo wa ubunge unatekemea utumishi mahususi kwa wananchi waliompa ridhaa.

Mheshimiwa Tarimba afikishiwe kuwa hekima ya kiongozi si sauti yake kwenye misafara, bali ni athari yake kwenye maisha ya waliompa dhamana.

Tuwaenzi wananchi wetu kwa kujikita katika mijadala ya kimsingi – inayobeba matumaini ya wengi – badala ya hoja zinazolenga hadhi ya wachache Kama wabunge.

Bendera ya kweli ya mbunge si ile inayopeperushwa juu ya gari, bali ni imani ya wananchi inayojitokeza kupitia matendo yako ya kila siku.
 
Viongozi wa Kiafrica....
Ubinafsi na umimi kwanza!
 
Tukiwatambua watapopolewa mawe maana hawa wabunge hawana chochote wanacho zalisha kwenye taifa hili ila ndio wanajilipa mamilion washenzi hawa
 
Ila huyu ponjoro amewafanya wapiga kura wa Jimbo la kinondoni kuonekana wapumbavu sana.

Alafu unakuta jitu kama hili linapewa kura Tena, watu wa kino hovyo sana.
 
Hiyo nayo ni habari? Acha husda kagombee na wewe km unaona number ni dili kubwa hivyo. Mbn watu wameandika majina yao kwenye plate number? Kinachokusumbua ni umaskini na roho mbaya
 
Ila huyu ponjoro amewafanya wapiga kura wa Jimbo la kinondoni kuonekana wapumbavu sana.

Alafu unakuta jitu kama hili linapewa kura Tena, watu wa kino hovyo sana.
Watu wa Kinondoni ni wajanja wamechagua mjanja siyo we mshamba umeingia mjini juzi, nenda kagombee wewe tuone
 
Kwani Wananchi wa Kinondoni hawana changamoto zozote akawasemea?
 
'Plate number' inaweza kuboresha maisha ya mpiga kura, kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…