Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi, mbunge huyo aliwahutubia wale wanaokandamiza haki, polisi wanaonyanyasa raia, watekaji, walanguzi wanaonyonya wakulima, wajiri wanaokandamiza wafanyakazi na wengine wanaokandamiza wanyonge.
Alisema baadhi ya watu wamezoea kudanganya, hasa vijana, kwa kuwaambia mikopo ipo ilhali inaishia matumboni mwao. Alisisitiza kuwa vijana wanastahili kupata mikopo na kuwataka wale wanaokandamiza wanawake, vijana na wazee waache tabia hiyo.
“Leo nawapa majibu yao. Maneno yote ninayosema, walioniituma ni mabosi zangu, wananchi wa Tunduru. Mimi kamwe sitaogopa binadamu, nitaendelea na mapambano ya kudai haki. Ndiyo msimamo wangu,” alisema Ado kwa sauti kali huku akiinua ngumi.
Aliongeza kuwa wananchi wamemwambia aongeze “moto” katika kazi yake. Kuhusu kero alizopokea, alizigawa katika makundi matatu. Kundi la kwanza ni mambo madogo madogo kama choo kumeharibika, bomba au mota imeharibika, na upungufu wa vitanda vya kujifungulia hospitalini, ambavyo anaweza kushughulikia kwa haraka.
Kundi la pili ni mambo yanayowezekana lakini yanahitaji mchakato. Alisema atachukua hoja hizo, kukaa na wataalamu, nyingine kuzipeleka wizara na nyingine Bungeni ili zifanyiwe kazi.
Ado alihitimisha kwa kuomba dua nyingi na kuwahakikishia wananchi kuwa kama walivyofanikiwa kwenye uchaguzi, pia changamoto zote zitapita salama.