Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Geita, Rose Busiga amegaragara chini wakati akimuombea kura Rais Samia Suluhu Hassan na Naibu Waziri Mkuu, Doto Biteko wakati wa mkutano wa hadhara katika kijiji cha Bufanka kilichopo wilayani Bukombe.
Akiomba kura hizo kwa lugha ya Kisukuma, mbunge huyo amesema anaibariki ardhi hiyo na hilo ni agano na wannachi ili wakati utakapofika wasiache kumpigia kura Rais na Naibu Waziri Mkuu ifikapo Oktoba 2025.
Mbali na kuomba kura, pia mbunge huyo amesema tayari wanawake wamechanga fedha kwa ajili ya kumchukulia Rais Samia fomu ya kugembea urais na kumuomba Biteko wakati utakapofika asichukue fomu kwa kuwa wanawake wa Geita watamchukulia na akishaijaza watairudisha wenyewe.
Uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais, wabunge na madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
===
Pia soma:
- Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025