Mbunge Agnes Marwa: Wananchi wa Mkoa wa Mara walipwe fidia ya ardhi yao

Mbunge Agnes Marwa: Wananchi wa Mkoa wa Mara walipwe fidia ya ardhi yao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. AGNES MARWA AISHAURI WIZARA YA MADINI, WANANCHI WALIPWE FIDIA ZAO

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Mhe. Agnes Marwa amechangia bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akisisitiza sana wananchi wa Mkoa wa Mara walipwe fidia ya ardhi yao ambayo inatumika katika uwekezaji wa dhahabu.

"Naiomba Serikali iwaangalie sana wachimbaji wadogo kwa kuwa, hali ya ajira ni mbaya sana katika taifa letu, kwa kuwa wachimbaji wadogo wamejitolea na kujiajiri wenyewe basi ni vyema wakaangaliwa kwa jicho la pekee" - Mhe. Agnes Marwa, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara

"Kuna maeneo yamechukuliwa na wawekezaji wakubwa ambayo yamekaa muda mrefu bila kufanyiwa kazi na yamesharudishwa Serikalini, ni vyema Serikali ikaona namna ya kuwagawia maeneo hayo wachimbaji wadogo ili nao waweze kufaidika na 'Kasungura ka Taifa' lao la Tanzania" - Mhe. Agnes Marwa, Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mara

"Ni vyema yakaangaliwa maeneo yote ambayo wachimbaji wadogo wadogo wanayatumia kwa uchimbaji na yakafikishiwa Umeme, hili limekuwa ni tatizo la muda mrefu hususan katika Mkoa wa Mara kwenye wanayatumia za Musoma, Bunda, Tarime. Ni vyema wachimbaji wadogo wakaangaliwa kwa jicho la pekee" - Mhe. Agnes Marwa, Mbunge Viti maalum Mkoa wa Mara.

FuzZs8KXgAAelY7.jpg
 
Back
Top Bottom